Na Baraka Mpenja
Bondia
Francis Cheka ametamba kumchabanga mpinzani wake Thomas Mashali ambaye
ni bingwa wa uzito wa Middle ukanda wa afrika mashari na kati (ECAPBA)
watakapokutana katika pambano la kutetea ubingwa wa afrika mei mosi PTA
jijini Dar es salaam.
Akizungumza
kutoka mkoani Morogoro alipoweka kambi yake, Cheka alisema yeye hataki
maneno mengi ila shughuli ni siku ya pambano ambapo Mashali lazima
akione cha mtema kuni.
“Kupitia
matndao wa Fullshangwe niwahakikishie watanzania na mashabiki wangu
kuwa naendelea kujifua vilivyo hapa Morogoro na nitakapo panda ulingoni
wengi wananijua kazi yangu”. Alisema Cheka.
Cheka
alisema siku zote maandalizi yake ni mazuri na watu wa Morogoro
wanamwamini sana na ndio maana anajiandaa kuwapa raha zaidi siku hiyo.
“Maneno
anayoongea Msahali waliongea akian Maugo, Kaseba na wengine, lakini
kazi yangu nadhani mnaiona jamani, Mashali haniwezi ingawa mchezo wa
masumbwi hauna mwenyewe”. Alijitapa Cheka.
Refarii
wa mpambano huo wa kukata na shoka atakuwa ni John Shipanuka kutoka
nchini Zambia ambaye alilisimamia pambano kati ya Francis Cheka na Mada
Maugo mwaka jana kwa ustadi mkubwa.
Shipanuka
ni Afisa Ugavi katika jeshi la Jamhuri ya Watu wa Zambia na ana ujuzi
mkubwa wa kusimamia mapambano ya ngumi ya kimataifa.
Aidha,
majaji wa mpambano huo ni Daudi Chikwanje kutoka Malawi ambaye ndiye
Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi Cha Malawi na ambaye anakuwa jaji namba
moja. Steve Okumu wa Kenya ambaye anakuwa jaji namba mbili na Ismail
Sekisambu wa Uganda ambaye anakuwa jaji namba tatu. Msimamizi mkuu wa
mpambano huo ni Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi.
Hii
ni mara ya pili kwa bondia Francis Cheka kutetea ubingwa wake tangu
amsambaratishe kwa TKO bondia machachari Mada Maugo katika mpambano
uliofanyika mwaka jana mwezi wa Aprili katika ukumbi wa PTA jijini Dar
Es Salaam.
0 comments:
Post a Comment