Mabondia
Francis Cheka na Thomas Mashali wanataraji kupima uzito hapo kecho tayari kwa
kupanda ulingoni mei mosi mwaka huu kuwania ubingwa wa IBF Africa ambao Cheke
ni bingwa mtetezi.
Rais
wa kampuni ya ngumu za kulipwa Tanzania
na mratibu wa pambano hilo Yasin Abdallah “Ustadhi” ameiambia MICHEZO
BOMBA! Kuwa maandalizi kwa ajili ya zoezi hilo yamekamilika na tayri mabondi
wate wapo jijini Dar es salaam.
“Wanaume
wote wapo Dar na hapo kesho wanapima uzito, hakika mbwembwe za mashabiki wa mabondia
hawa zinaleta rah asana, wengine wakimfananisha Cheka na Real Madrid na
Barcelona kuwa atapigwa katika raundi ya nne, lakini tusubiri”. Alisema Yasin.
Yasin
alisema mshindi wa pambano hilo la ubingw wa IBF litakalopigwa ukumbi wa
Sabasaba PTA jijini Dar es salaam atazawadiwa gari aina ya Noah.
Yasin
aliwataka mashabiki wa masumbwi na wapenzi wa michezo kwa ujumla kujitokeza kwa
wingi kesho kutwaa kwa ajili ya kushuhudia pambano la kufa mtu kati ya miamba
Cheka na Mashali.
|
Home
»
»Unlabelled
» CHEKA NA MASHALI KUPIMA UZITO KESHO
Monday, April 29, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment