Na Baraka Mpenja
Chama cha mchezo wa netiboli Tanzania
CHANETA kimetangaza kuongeza muda kwa mikoa wanachama wake ili kukamilisha
suala la uchaguzi na kulipia ada ya uanachama.
ROSE MKISI |
Akizungumza na mtandao huu, kaimu
katibu wa CHANETA Rose Mkisi amesema, wameongeza siku mpaka aprili kumi mwaka huu, siku ambayo watatoa
vitambulisho kwa wajumbe wa mkutano mkuu na uchaguzi wa viongozi.
Mkisi alisema mikoa wa katavi na
Tabora tayari imeshakamilisha uchaguzi wake na kulipa ada ya uanachama.
“Tumeamua kuongeza muda kwa wanachama
wetu ili wafanye uchaguzi, lakini maandalizi kwa ujumla yanakwenda vizuri, huku
tukiwasubiri baraza la michezo la Tanzania BMT kutoa fedha walizotuahidi kwa
ajili ya kufanya mkutano mkuu pamoja na uchaguzi wa viongozi”. Alisema Mkisi.
Kiongozi huyo alisisitiza kuwa mwaka
huu wanataka kufanya uchaguzi huru na
haki, na kama mtu yeyote atakosa kitambulisho hataruhusiwa kushiriki.
Pia Mkisi alisema hakuna wa
kulalamika mwaka huu, kwani watu waliochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi wamebakia wale wale.
Katibu huyo alitaja watu walioomba
nafasi ya mwenyekiti kuwa ni wajumbe wawili, nafasi ya makamu mwenyekiti pia kuna wajumbe
wawili , kwa upande wa nafasi ya ujumbe
wa kamati ya utendaji ya CHANETA wapo watu tisa, huku nafasi ya mweka hazina akiwepo mtu mmoja.
“Hakuna wa kulaumu, viongozi wa chama
tumetumia muda mrefu sana kutangaza uchaguzi huu, kama mtu atajitokeza kulaumu
atakuwa na jambo lake la siri, lakini sisi tunasisitiza kuwa waliochaguliwa
kuingia katika uchaguzi huo ni wale wale kwani watu hawakujali”. Aliongeza
Mkisi.
Mkisi alisema mchezo wa Netiboli ni
muhimu kwani unafanya vyema kimataifa tofauti na michezo mingine hususani
mchezo wa soka ambao unapewa kipaumbele kikubwa na viongozi wa serikali sanjari
na wadau wa michezo kwa ujumla.
Aliongeza kuwa ni wakati mwafaka kwa
watanzania kuthamini na kutupia jicho la tatu katika mchezo wa netiboli ili
bendera ya taifa iendelea kupepea medani
Usaili kwa wale waliomba nafasi
mbalimbali za uongozi utafanyika aprili
18 huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika aprili
20 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment