Kocha wa muda wa klabu ya CHELSEA , RAFA BENITEZ
amesema wachezaji wake waliokuwa
nje ya dimba kwa muda wa wiki tatu
ASHLEY COLE na GARY CAHILL tayari wamerudi kikosini
kujiunga na wenzao kwenye mazoezi
yanayoendelea kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya LIVERPOOL
utakaopigwa kesho dimbani ANFIELD jijini
LIVERPOOL.
Nyota hao wamekuwa nje ya dimba kwa
takriban wiki tatu mfululizo kufuatia
maumivu yaliyokuwa yanawasumbua, lakini
sasa imedhibitika kuwa wamerudi uwanjani
toka jana na tayari kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi
ya watoto BRENENDA ROGERS utakao pigwa hapo kesho
Kwa upande wake BENITEZ amesema kurudi kwa ASHLEY na CAHILL
uwanjani ni jambo zuri sana kwa klabu hiyo, kwani mchezo wa kesho ni muhimu sana na unahitaji
timu iliyokamilika.
Pia alipo ulizwa kuhusu hali ya
mshambuliaji JOHN TERRY ambaye alifungia
timu yake magoli mawili dhidi ya FULHAM ijumaa iliyopita, bosi huyo amesema ,TERRY
yuko fiti na anaendelea na mazoezi na wezake kama kawaida.
Vilele vijana wawili wa BENITEZ , EDEN HAZARD na JUAN MATA
hapo jana wametangazwa kushiriki
katika kinyng’anyiro cha mchezaji bora wa FA msimu huu.
AC MILAN: TELI APUNGUZIWA ADHABU.
Mario baloteli. |
Wakati adhabu ya mshamuliaji wa
zamani wa klabu ya MANCHESTER CITY
lakini anayekipiga kwa sasa katika klabu ya AC MILAN,
MARIO BALOTELI ikipunguzwa kutoka kukosa mechi tatu hadi kukosa mechi mblili baada ya kutumia lugha ya matusi kwa refa
msaidizi uwanjani wakati timu yake
ikikabiliana na FIORENTINA, bado nyota huyo hatakuwa miongoni mwa wachezaji
kumi na mmoja watakao shuka dimbani kumenyana na JUVENTUS
Juma pili hii.
TELI, alionyeshwa
kadi ya manjano kwa mara ya nne msimu huu wakati timu yake ikicheza dhidi
ya FiORENTINA ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya
magoli 2-2, Kitendo hicho kilimfanya
nyota huyo kupumzishwa mechi moja nje, lakini baadaye aliongezewa adhabu ya
kukosa mechi zingine mbili baada ya kutoa lugha
ya matusi kwa msadizi wa muamuzi wa kati katika mchezo huo.
Lakini
baada ya rufaa ya AC MILAN kupita,mshambuliaji huyo atakosa mechi mbili badala
ya tatu huku pia akilazimika kulipa fainai ya
paundi 20,000.
REAL MADRID
Rafael Varane. |
Akiwa na umri wa miaka 19, mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu
wa Lens amepata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza hapo dimbani BERNABEU chini ya kocha huyo wa
zamani wa CHELSEA, na mekuwa akionyesha
soka la hali ya juu.
Akiongea na wana habari kinda aliendela kusema kuwa licha ya juhudi zake
binafsi katika kuboresha kiwango chake,
anamshukuru sana MORINHO kwa kumjengea ujasiri wa hali ya juu katika
soka.
Francis
Kivuyo www.goal.com
0 comments:
Post a Comment