UWANJANI
White Hart Lane, Tottenham Hospur leo wameitandika Manchester City Bao
3-1 na kujipa matumaini ya kuwemo kwenye 4 Bora ili kucheza ligi ya
mabingwa Ulaya Msimu ujao na pia kuwakata maini Man City matumaini yao
finyu ya kutetea Taji lao la Ubingwa ambalo kesho Usiku linaweza
kuchukuliwa na Mahasimu wao Manchester United ikiwa wataifunga Aston
Villa Uwanjani Old Trafford.
City
walitangulia kufunga Bao mapema kupitia Samir Nasri katika Dakika ya 5
lakini Bao 3 ndani ya Dakika 6 na Sekunde 20 kuanzia Dakika ya 75
zilizofungwa na Clint Dempsey, Jermain Defoe na Gareth Bale
ziliwasambaratisha Man City.
Tottenham
sasa wamefungana Pointi na Chelsea iliyo nafasi ya 4 lakini wanaweza
kuishusha Arsenal iliyo nafasi ya 3 ikiwa watashinda Mechi yao moja
waliyonayo mkononi.
VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Assou-Ekotto, Sigurdsson, Dembele, Parker, Bale, Dempsey, Adebayor
Akiba: Friedel, Huddlestone, Naughton, Defoe, Holtby, Livermore, Caulker.
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Toure, Barry, Milner, Tevez, Nasri, Dzeko
Akiba: Pantilimon, Lescott, Sinclair, Kolarov, Javi Garcia, Aguero, Kolo Toure.
Refa: Lee Mason
0 comments:
Post a Comment