![]() |
Messi aomba miujiza itokee,katika
marejeano
Mabingwa wa mara nne wa
michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya,Bayern Munich ya Ujerumani wamejiweka
mazingira ya mazuri ya kutinga fainali baada ya kuinyuka Barcelona ya Hispania
kwa magoli 4 – 0.
Hiyo ilikuwa nusufainali ya
kwanza ya michuano hiyo maarufu
ulimwenguni.
Katika mechi ya iliyochezwa katika dimba la Allianz Arena
ilishuhudia wenyeji wakipata goli la kwanza kupitia kwa Thomas Mueller dakika
25 na Super Mario Gomez dakika ya 49 huku mengine yakiwekwa kimiani na Arjen
Robben na Mueller kwa mara nyingine.
Sasa Barcelona watahitaji
ushindi wa magoli 5 – 0 katika mechi ya marejeano ili kutinga hatua ya fainali.
Mshambuliaji nyota wa timu
hiyo Lionel Messi amesema timu yake
inahitaji miujiza ili kushinda katika
mechi ya marejeano huku akisema ni moja ya kipigo cha aibu kuwakutokea katika
kipindi cha ushiriki wao wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.
“Magoli 4 – 0 ni pengo kubwa
kulifidia katika mechi ya marejeano,itakuwa mechi ngumu kwetu”alisema Messi
Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes amewaonya wachezaji wake kutojiamini kupita kiasi
kwani kuna kibarua cha marejeano chenye dakika 90 zingine kama walizocheza
Allianz Arena.
Mshambuliaji Arjen Robben wa
Bayern Munich asema “yaani huwezi
kuamini ni kama wazimu vile huwezi kuamini tumeshinda magoli 4 – 0 kwa timu
iliyotawala Ulaya kwa miaka ya hivi karibuni”

Barcelona wameruhusu wavu wao
kuguswa mara nne katika mechi ya Champions League kwa mara ya kwanza tangu
walipofungwa 4-2 na Chelsea katika hatua ya 16 bora Machi 2005.
Kwenye michuano yote ambayo BARCA imeshiriki hivi karibuni haijawahi kucharazwa kwa magoli 4-0 tangu Getafe ilipowatandika kwa bakora kama hizo katika kombe la mfalme mwaka 2007.
Klabu
ya kwanza kuichapa Barcelona 4 – 0 katika michuano ya Ulaya ilikuwa ni Dynamo Kiev
ya Ukraine katika hatua ya makundi mnamo
1997.
Kwa
historia tu hakuna timu iliyowahi kuchapwa idadi kama hiyo ya mabao katika
michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya ikafanikiwa kusonga mbele…….…. Je Barcelona
ni mwisho wa enzi?Hapo ni muda utatuambia , vuteni subira mechi ya marejeano
Nou Camp nyumbani kwa Barcelona hali itakuwaje? ……..
REAL MADRID,DORTMUND VITANI USIKU WA LEO
Mara baada ya Miamba ya
Hispania Barcelona kunyooshwa na wajerumani,Bayern Munich sasa ni zamu ya
mahasimu wao Real Madrid kupambana na wajerumani wengine Borussia Dortmund wakicheza nyumbani Signal Iduna Park usiku wa leo.
0 comments:
Post a Comment