>>WADAI: ‘HAJUI SHERIA ZA GEMU!!!’

Barca hawakufurahishwa na uchezeshaji wa
Stark na wamedai Refa huyo kutoka Germany ‘hajui Sheria za Gemu’ kwa
kuruhusu Mpira uendelee wakati Wachezaji wawili wa Barca, Javier
Mascherano na Jordi Alba, walikuwa wamelala chini baada ya kugongana
wenyewe.
Barca wamedai Refa huyo alipaswa
kusimamisha Mpira wakati huo na pia hakupaswa kulikubali Bao la kwanza
la PSG ambalo alifunga Zlatan Ibrahimovic wakati akiwa Ofsaidi.
Msemaji wa Barcelona, Toni Freixa,
amesema Klabu yao imewaandikia UEFA kufuatia mlolongo wa makosa ya Refa
huyo ikiwa dhahiri kuwa hakufuata Sheria za Soka.
Uamuzi wa kumshitaki Refa huyo UEFA ulichukuliwa na Barcelona baada ya Bodi ya Klabu hiyo kukutana Siku ya Alhamisi.
Msimu huu, Wadau wengi wamekuwa
wakilalamika kuhusu uchezeshaji wa Marefa usiokuwa makini hasa baada
Mchezaji wa Manchester United, Nani, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu Man
United walipofungwa 2-1 na Real Madrid lakini tukio kama la Nani
lilifanywa mara mbili na Wachezaji wa Real Madrid walipoifunga
Galatasaray Bao 3-0 juzi Jumanne lakini Wachezaji wa Real hawakupewa
Kadi yeyote.
KUTOKA SOKA IN BONGO
0 comments:
Post a Comment