Na Baraka Mpenja
Mechi
kali ya kombe la shirikisho baina ya Azam fc ya Tanzania dhidi ya timu
ya jeshi la Morroco AS FAR Rabat imemalizika uwanja wa taifa jijini Dar
es salaam kwa matokeo ya suluhu pacha ya bila kufungana.
Katika
mchezo huo timu zote mbili zimekosa nafasi nyingi za kutia mpira
nyavuni huku dakika za mwisho waarabu wa Morroco wakijiangusha mara kwa
mara kutaka suluhu ugenini.
Azam
FC imeshindwa kutamba katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Emile
Fred kutoka Shelsheli na endapo ingeshinda ingejiwekea mazingira mazuri
ya kusonga mbele hatua ya makundi.
Sasa Azam watakuwa na kibarua kizito huko kaskazini mwa Afrika wiki mbili zijazo kwani watahitaji ushindi tu na si vinginevyo.
Kama
wawakilishi hao watanzania watahitaji kujaribu bahati yao watahitaji
kulazimisha suluhu ugenini ili sheria itumike, lakini kama watahitaji
kusonga mbele ndani ya dakika 180 watalazimika kupata matokeo ya
ushindi.
Katika
dakika ya mwisho ya mchezo huo nyota wa Azam Kipre Herman Tchetche
alipiga bunduki moja iliyogonga mtambaa panya na baada ya hapo mwamuzi
Fred alipuliza kipenga cha mwisho kuashiria ngoma imemalizika.
Akiongea
baada ya mechi hiyo kocha mkuu wa Azam fc, mwingereza Sterwat John Hall
alisema ni matokeo mabaya kwao kwani wanahitaji kujipanga vizuri mechi
ya marudiano.
“Tumepoteza
nafasi nyingi, bahati haikuwa yetu lakini tunaweza kubadili matokeo
tukienda kwao kwani katika soka kila kitu kinawezekana”. Alisema Hall.
Kocha huyo aliongeza kuwa timu yake ilicheza vizuri na kwa umakini sana lakini bahati haikuwa yao kwa siku ya leo.
0 comments:
Post a Comment