Na Baraka Mpenja
Siku
moja baada ya klabu ya Azam fc maarufu kama lambalamba kushindwa
kuwatungua wanajeshi la Morroco AS FAR Rabat katika mchezo wa kwanza wa
raundi ya tatu kombe la shirikisho barani Afrika, wadau wameendelea
kutoa maoni yao juu ya matokeo hayo na kusema wawakilishi hao wa
Tanzania wanaweza kufanya vizuri mechi ya Marudiano wiki mbili zijazo
nchini Morroco.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Fullshangwe wadau
hao walisema Azam inatakiwa kujiandaa sana kutokana na uzoefu
unaoonesha kuwa timu nyingi za waarabu zina tabia ya kutafuta sare ama
suluhu ugenini na hatimaye kumaliza kazi wakirudi kwao.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa shirikisho la soka Tanzania Sunday Bato Kayuni alisema
watanzania wengi hawakutegemea matokeo ya jana ingawa ukweli ulikuwa
pale pale kuwa, FAR Rabat ni timu nzuri yenye uzoefu mkubwa wa
mashindano ya Afrika kuliko Azam ambao ndio mara ya kwanza kushiriki
michuano ya kimataifa.
Kayuni
alisema Azam ilicheza kwa presha kubwa kwani ilikuwa inahitaji matokeo
ya nyumabi ili kupata unafuu katika mchezo wa marudiano, lakini waarabu
waliwahimili vizuri na kulazimisha suluhu pacha ya bila kufungana.
“Bado
timu yetu ina faida ya kusonga mbele, Rabat wao watahitaji ushindi hata
wa bao moja, wakati Azam wanahitaji sare ya magoli yoyote ama ushindi,
na kama watapata goli moja ugenini itawagharimu wamorroco, kila kitu
kinawezekana, kinachotakiwa ni mwalimu na wachezaji kujipanga vizuri na
kuamini wanaweza kufanya vizuri”. Alisema Kayuni.
Kayuni
aliongeza kuwa michezo ya awali Azam walionekana kutokucheza vizuri
sana uwanja wa nyumbani kutokana na kuhitaji matokeo ya ushindi na
kuwafurahisha mashabiki waliofurika uwanjani, lakini mechi za ugenini
walipata ushindi mnono, hivyo hata Morroco wanaweza kupata ushindi mnono
pia.
Kwa
upande wake kocha wa zamani wa African sports ya Tanga, Mjumbe wa kamati
ya ufufundi ya simba na mwalimu wa soka la vijana TFF, John William
“Del Piero” alisema timu ya Rabat ni ngumu sana na wana ujanja mwingi wa
kulazimisha matokeo wanayoyahitaji.
Piero
alisema timu ambazo Azam ilikutana nazo awali hazikuwa ngumu kama timu
ya jana, hivyo kinachotakiwa kwa wachezaji ni kujitambua kuwa nini
wanataka kufanya pamoja na kusikiliza maoni ya kocha wao sanjari na
walimu waliobobea katika mchezo wa soka.
“Azam
ina wachezaji wazuri na mwalimu mzuri, endapo watajipanga barabara
wanaweza kusonga mbele, lakini wajiandae kwa hujumu zozote zile kwa
sababau waarabu wanapokuwa ugenini wanapenda kufanyia haki lakini wakiwa
kwao wana mambo ya kipuuzi sana”. Alisema Piero.
Naye
katibu mkuu wa zamani wa shirikisho la soka Tanzania, Fredrick
Mwakalebela alishauri Azam kukaa chini na kuangalia wapi waliteleza
katika mchezo wa nyuambi kwani waarabu tabia yao ni kumaliza mchezo
wakiwa kwao.
Mwakalebela
aliongeza kuwa katika mchezo wa jana wawakilishi hao wa Tanzania katika
michuano ya kimataifa walicheza vizuri na kupoteza nafasi muhimu
kufunga, lakini hilo ndio soka labda bahati yao itakuwa Morroco.
“Kipre
Tchetche alipiga shuti kali dakika ya mwisho lakini liligomba mtamabaa
panya, hakika lilikuwa bao kwa Azam, mimi nafikiri ushinid katika mchezo
wa jana ungepatikana endapo wangetulia dakika za mwanzo”. Alisema
Mwakalebela.
Katibu
huyo wa zamani wa TFF aliwatakaka Azam na watanzania kwa ujumla
hususani waliopo kule Morroco ingawa sio wengi kuwapa sapoti kubwa
matajiri hao wa Tanzania ili wakienda huko wapate motisha ya kucheza
vizuri na kuvumilia hujuma za waarabu ambao ni kawaida yao.
0 comments:
Post a Comment