Habari zinasema kwamba, kocha Arsene Wenger anaihofia Chelsea kwa namna ilivyopanga kujisuka upya.
The Gunners wamekuwa wakimfuatilia
Jovetic, mwenye umri wa miaka 23, tangu mwaka 2011 na wakati klabu hiyo
ya Serie A inamthaminisha kwa kiasi cha Pauni Milioni 25, Arsenal —
ambayo ina bajeti ya Pauni Milioni 70 za usajili, inataka ipunguziwe bei
ya kumnunua mchezaji huyo

Anatakiwa sana: Arsenal iko tayari kumwaga mpunga kwa ajili ya Stevan Jovetic
Hatua ya klabu hiyo kufanya jitihada za
mapema kumnasa Jovetic ni dalili nzuri, haswa ikizingatiwa Manchester
City na Juventus zote zinamtaka mshambuliaji huyo. Dili lolote
litategemea na Arsenal kama itafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Wenger, pia anatazamia kumsajili kipa mpya wa kwanza, na amekuwa akimmulika mlinda mlango wa Hamburg, Rene Adler tangu Machi.
MICHEZO BOMBA inatambua msaka vipaji mkuu
wa Arsenal, atatoa uamuzi wa mwisho juu ya kipa huyo mwenye umri wa
miaka 28, baada ya mechi ya Jumapili dhidi ya Schalke. Arsenal inaona
kulikoni kutoa Pauni Milioni 15 kuwanunua ama kipa wa Stoke, Asmir
Begovic au wa Sunderland, Simon Mignolet, bora kutoa Pauni Milioni 8
kumnasa kipa huyo Mjerumani.
Wenger anataka kuboresha kikosi chake
kujiandaa kupambana na Chelsea ambayo iko mbioni kuwasajili kiungo
mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Andre Schurrle na mshambuliaji wa
Atletico Madrid, Radamel Falaco.

Mikono salama: Arsenal pia inamtaka kipa wa Hamburg, Rene Adler

Woga: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anaihofia Chelsea ilivyopanga kumwaga mpunga kusajili
Wenger amesema: "NInahofia na kitu
wanachoweza kufanya Chelsea mwishoni mwa msimu. Tunatakiwa kujiandaa kwa
ajili yao kwa kuwa moja ya klabu zilizowekeza.".
Wakati huo huo, Alex Oxlade-Chamberlain amesema amechoka maisha ya benchi.
Winga huyo amecheza mechi 11 tu katika kikosi cha kwanza Arsenal kwenye Ligi Kuu msimu huu.

Wawili matatizo: Chelsea inatumai kumsajili Andre Schurrle (juu) na Radamel Falaco (chini)

0 comments:
Post a Comment