Na Baraka Mpenja wa msaada wa sportsmail.com
Baada
ya kutwaa ubingwa wa 20 na klabu ya Manchester United, Bosi wa
mashetani hao wekundu, Sir Alexandar Chapman Ferguson “Kibabu Fergie”
ametajawa tena katika tuzo nyingine ya kocha tajiri zaidi katika soka la
England kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na gazeti la Sunday Times.
Ferguson
ameshinda taji ya kuwa kocha tajiri zaidi akifuatiwa katika nafasi ya
pili na aliyekuwa kiungo wake Old Trafod Roy Keane huku mzee Arsene
Wenger akiwa nafasi ya tatu.
Kibabu ametajwa kuwa kocha tajiri zaidi England akiwa na kitita cha pauni milioni 34 katika akaunti yake.

Tuzo nyingine: Sir Alex Ferguson kocha tajiri zaidi kwa mujibu wa orodha ya gazeti la Sunday Times
Roy Keane alitengeneza pesa nyingi akiwa mchezaji na sasa anapata pesa nyingi tena akiwa mtangazaji wa ITV



Naye
kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson ambaye ana mkataba wa
pauni milioni 3 kwa mwaka na chama cha soka England ameingia kumi bora
akiwa na kitita cha pauni milioni 12, lakini anazidiwa na kocha
aliyemrithi mikoba yake Sven Goran Eriksson aliyejikusanyia pauni
milioni 16.
Kocha Manchester City Roberto Mancini na wa Ireland Giovanni Trapattoni wameingia pia katika orodha hiyo.
Pia
kocha wa muda wa Chelsea Rafa Benitez yupo kwenye orodha hiyo akiwa na
kitita cha Pauni milioni 12 licha ya mkataba wake kuwa mwishoni.

MAKOCHA TAJIRI ZAIDI WA SOKA(Pamoja na makocha wa zamani wa timu za Uingereza)
Ranking | Name | Team | 2013 wealth | 2012 wealth |
1 | Sir Alex Ferguson | Manchester United | £34m | £32m |
2= | Roy Keane | Ex Ipswich Town and Sunderland | £29m | £29m |
2= | Arsene Wenger | Arsenal | £29m | £26m |
4= | Roberto Mancini | Manchester City | £21m | £18m |
4= | Giovanni Trapattoni | Ireland | £21m | £20m |
6 | Sven-Goran Eriksson | Ex England and Leicester City | £16m | £16m |
7= | Steve Bruce | Hull | £14m | £14m |
7= | Mark Hughes | Ex-QPR | £14m | £11m |
9 | Harry Redknapp | QPR | £13m | £12m |
10= | Rafa Benitez | Chelsea | £12m | New |
10= | Roy Hodgson | England | £12m | £11m |
10= | Martin O’Neill | Sunderland | £12m | £10m |
Wakati huo huo Lewis Hamilton
ametajwa kuwa dereva mwenye kitita kikubwa kuliko wote wa michezo ya
Fumula One ambapo ana kitita cha Pauni milioni 60.
Nafasi ya pili imeshikwa na Jenson Button ambaye ana kitita cha pauni milioni 5

Madereva tajiri zaidi wa F1 wazaliwa wa Uingerza
Ranking | Name | F1 Team | 2013 wealth | 2012 wealth |
1 | Johnny Dumfries | Lotus | £110m | £110m |
2 | Eddie Irvine | Ferrari | £83m | £80m |
3 | Lewis Hamilton | Mercedes | £60m | £55m |
4 | Jenson Button | McLaren | £58m | £53m |
5 | Jody Scheckter | Ferrari | £57m | £60m |
6 | David Coulthard | McLaren | £53m | £50m |
7 | Nigel Mansell | Williams | £50m | £50m |
8 | Sir Jackie Stewart | Tyrrell | £42m | £42m |
9= | Damon Hill | Williams | £19m | £19m |
9= | Jonathan Palmer | Tyrrell | £19m | £22m |
0 comments:
Post a Comment