JUMA PINTO-MWENYEKITI TASWA |
Rais
wa AIPS,Gianni Merlo raia wa Italia aliwapa fursa viongozi wa vyama vya
waandishi wa habari za michezo wa Afrika kuwasilisha changamoto
mbalimbali zinazovikabili vyama vyao, lakini kati ya hizo changamoto
waitaje moja ambayo wanataka AIPS isaidie kuwapa msaada.
Tunashukuru
Merlo kwanza alivutiwa sana na namna Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA) kinavyofanya kazi zake na ushiriki wake wa
mikutano ya Dunia mara kwa mara, hali ambayo aliahidi yeye binafsi
kusaidia chama chetu kuboresha masuala ya kimsingi.
Kubwa
ambalo AIPS baada ya kuelezwa imesema italipangia utaratibu ni suala la
mafunzo kwa waandishi wa habari chipukizi na wanawake kwani hayo ni
baadhi ya mambo ambayo wenyewe wanayatilia mkazo na hasa baada ya
kujulishwa kuwa kuna wanahabari zaidi ya 50 wanawake hapa nchini
wanaofanya kazi kwenye masuala ya michezo.
Hata
hivyo ingawa TASWA iliomba isaidiwe mafunzo kwa wanachama wake wote kwa
kupatiwa wataalamu hasa wakati huu ambao kuna changamoto kubwa ya
teknolojia ya habari na mawasiliano, lakini AIPS imesema kwa mwaka huu
uwezo wake ni kwa waandishi wa habari za michezo chipukizi kupitia
programu inayoandaliwa na AIPS.
Lakini
Rais wa AIPS aliutaka ujumbe wa Tanzania utakapokuwa umerudi nyumbani
umuandalie mikakati hiyo kwa mafunzo ya wanawake ili ikiwekezekana
yafanyike kwa awamu katika kipindi cha miezi 18 kutegemea na idadi ya
wahusika na pia gharama zenyewe.
0 comments:
Post a Comment