Thursday, March 14, 2013


Picha na Bin Zubeiry

Kikosi cha Yanga

Na Baraka Kizuguto
KIKOSI cha Yanga jana kimeingia kambini katika hosteli zake zilizopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwnai, Dar es Salaam baada ya mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika katika Uwanja wa Mabatini, Kijitonyama, kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani, utakaofanyika Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Yanga, ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 45 na mabao 36 ya kufunga, itashuka dimbani Jumamosi kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mgumu zaidi.
Katika mchezo wa awali wa mzunguko wa kwanza, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, huku Ruvu Shooting ikitangulia kuongoza kwa mabao 2-0 hadi mapumziko, kabla ya kipindi cha pili Yanga kubadilika na kurudisha mabao yote na kuongeza bao la ushindi.
Kocha Mholanzi, Ernie Brandts amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri kuelekea mchezo wa Jumamosi, kwani wachezaji wote ni wazima na wana morali ya hali ya juu.
“Kila mchezo kwetu tunautazama kama fainali, kutokana na timu zote za Ligi Kuu katika mzunguko wa pili kubadilika, kila timu inahitaji ushindi, inahitaji kuonyesha ina uwezo, lakini kwa kuwa sisi ni bora, mwisho wa siku naamini timu yangu itaibuka na ushindi,” alisema beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi.
Wachezaji Kevin Yondan, Stefano Mwasyika hawakushiriki mazoezi ya jana kufuatia kuwa na matatizo tofauti. Yondani anasumbuliwa na tatizo la uvimbe wa kidole gumba cha mguu wakati Mwasyika alikua ana homa.
Beki Ladislaus Mbogo pia hakufanya mazoezi kufuatia kwenda hospital kufanyiwa upasuaji wa uvimbe katika shavu lake, kwa mujibu wa daktari wa timu Dr Nassoro Matuzya upasuaji huo umemalizika salama na mchezaji huyo anatarajiwa kuwa nje ya Uwanja kwa wiki tatu.
Wachezaji wote wameingia kambini jana, isipokuwa Mbogo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video