PICHA NA BIN ZUBEIRY |
Na Baraka Adson
Vinara wa ligi kuu Tanzania bara wamesema kauli mbiu yao toka watoke nchini uturuki walipoweka kambi kwa wiki mbili kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa ligi kuu bara ni "Ushindi katika mechi zote za mzunguko wa pili".
Afisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto ameimabia MATUKIO DUNIANI kuwa kila mechi ni fainali kwao na ndio maana wanajituma sana katika kila mchezo wa ligi kuu bara.
Kizuguto alisema wachezaji kuwa na uwezo wa kujielewa na utulivu ndani ya klabu ndio umewafanya wafikishe alama 45 kileleni baada ya hapo jana kuwabamiza wadogo zao Toto Africans ambao wapo nafasi ya 13 na wanang`ang`ana kusalia ligi kuu bao 1-0.
Kizuguto aliongeza kuwa baada ya ushindi wa hapo jana, wachezaji wote kesho wataanza mazoezi katika viwanja vya mabatini kijitonyama kujiandaa na mchezo wao wa machi 16 dhidi ya maafande wa Ruvu shooting wa Mkoani Pwani.
"Mechi yetu na Ruvu shooting ni ngumu kutokana na ubora wao, lakini hatuwaogopi na tunasimamia kauli yetu ya ushindi wa mechi zetu, hivyo tunaanza maandalizi kesho kuwavaa vijana hao wa pwani". Kizuguto alisema.
Pia aliwataka mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwapa "sapoti" katika mechi zote ili kunyakua ubingwa ambao unashikiliwa na watani zao wa jadi, wekundu wa msimbazi, Simba ambao baada ya ushindi wa leo wa 2-1 dhidi ya Coastal union wamefikisha alama 34 katika nafasi ya tatu.
0 comments:
Post a Comment