Na Baraka Mpenja
kwa msaaada wa Mtandao
Unapozungumzia
makipa bora katika ulimwengu wa soka kwa
sasa, ukisahau jina la mlinda mlango namba moja kwa muda mrefu wa Real Madrid
ya Hispania,Mhispania, Iker Casillas Fernández utakuwa umetenda dhambi kubwa kwa
wapenda michezo duniani.
Katika
kikosi cha Real Madrid kinachonolewa na kocha mwenye maneno mengi Mreno, Mario
Jose Dos Santos Ferlix Morionho, Casillas amekuwa chaguo la kwanza na nahodha
wa klabu hiyo kwa muda mrefu hali ambayo imemfanya ajijengee heshima kubwa
miongoni mwa wachezaji wenzake na mashabiki kwa ujumla.
Mlinda
mlango huyo anasifika kwa umahiri wake akiwa langoni kwani anafanya vitu vya
ajabu hasa timu yake inapohitaji ushindi muhimu.
Makala
hii inajaribu kumchambua kiundani mkali huyu wa Ulaya kwa kungalia historia
yake ya soka, baadhi ya mafanikioa machache kati ya mengi aliyopata na maisha
yake nje ya uwanja.
Casillas
alizaliwa mei 20, 1981 katika mji wa Móstoles, uliopo Hispania. Baba yake anaitwa
José Luis Casillas, mtumishi wa umma wizara ya elimu na mama yake anaitwa Carmen
Fernández González, mwanamitindo wa nywele.
Maisha ya soka ya nyota huyo yalianzia
katika klabu yake ya Real Madrid mwaka 1990.
Mwaka 1990-91 alianzia soka katika kikosi
cha vijana cha Real Madrid na mnamo novemba 1997 akiwa na miaka 16 alitajwa kwenye kikosi cha
kwanza cha klabu yake kukabiliana na klabu ya Rosenborg ligi ya mabingwa barani
ulaya.
Katika msimu wa 1998-99 alijumuishwa rasmi
kwenye kikosi cha wakubwa na kumkalisha benchi mlinda mlango wa wakati huo ,Bodo
Illgner.
Msimu unaofuata alimwondoa rasmi Illgner
kwenye kikosi cha kwanza na kuwa chagua nambo moja la Real Madrid huku
mashabiki wengi wakimkubali kwa asilimia kubwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa
kusimama langoni.
Mwaka 2000 aliyekuwa kipa mwenye umri
mdogo zaidi kuwahi kucheza fainali ya UEFA
wakati klabu yake ilipocheza dhidi ya Valencia, na kuibuka na ushindi wa
mabao 3-0 huku zikiwa zimepita siku nne
akitokea kusherekea siku ya kuzaliwa kwake.
Msimu wa 2001-2002 wa UEFA nyota huyo
alipoteza nafasi yake kwa kipa César Sánchez kuchukua mikoba yake, lakini
alipata bahati tena mwishoni mwa msimu huo baada ya kipa huyo kuumia dakika za
mwisho za mechi ya fainali baina ya klabu
yake dhidi ya Bayer Leverkusen ambapo Madrid waliibuka washindi kwa
mabao 2-1.
Msimu wa 2007-9 ulikuwa wa mafanikio
makubwa kwa mlinda mlango huyo baada ya kuisaidia klabu yake ya Real Madrid
kutwaa kombe la La 31 la ligi kuu nchini Hispania huku akifungwa mabao 32
katika mechi 36 alizosimama langoni.
Majira ya joto ya usajili ya 2009 barani
ulaya, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa klabu kubwa duniani wakiwemo
matajiri wa England, Manchester city walitangaza kumtaka nyota huyo kwa ada ya
uhamisho wa pauni milioni 129, lakini Madrid walikanusha uvumi huo na Casillas
mwenyewe alikaririwa akisema hayuko tayari kuihama klabu yake hiyo aliyoichezea
toka utotoni.
Maajabu ya Casillas yalionekana msimu wa
2009-10 oktoba 4 katika mchezo wao dhidi ya Sevilla baaada ya kuokoa bao la
wazi akitokea upande mmoja wa goli na kuruka upande wa pili na kumnyima nafasi ya
kufunga mshambuliaji Diego Perotti ambaye mpaka sasa anaota bao hilo.
Baada ya kuokoa kimaajabu bao hilo,
alipokea pongezi kutoka kwa kipa mwenzake mzaliwa wa Hispania lakini raia wa
Uingereza Gordon Banks ambaye alisema nyota huyo kama ataendelea kucheza kwa kiwango
kile atakuwa miongoni mwa makipa bora
zaidi kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka.
Msimu wa 2011-12, Casillas alishinda Tuzo
ya kipa bora ya IFFHS
iliyomfanya kuwa kipa wa pili kushida tuzo hiyo baada ya Gianluigi Buffon kushinda mara nne mfululizo na yeye kushinda mara nne
pia.
Mwezi mei 2012, Casillas aliingoza klabu yake kutwaa
ubingwa wa 5 wa La Liga akiwa kama nahodha wa klabu baada ya kuifunga Bilbao
3-0.
Msimu wa 2012-2013 ambao unaelekea
ukingoni Casillas ameshinda tuzo ya IFFHS akiwa mlinda mlango bora kwa mara ya
tano mfululizo na kumfanya kuwa mlinda mlango pekee kutwaa tuzo hiyo mara
nyingi.
Mbali na mafanikio hayo katika ngazi
ya klabu, Casillas pia amefanikiwa kwa kiwango kikubwa akichezea timu ya taifa
ya Hispania.
Kwa mara ya kwanza kuichezea timu ya
taifa ni mwaka 1997 alipocheza kikosi cha vijana chini ya miaka 17 na yeye
akiwa mchezaji mdogo kuliko wote akiwa na miaka 16 fainali za kombe la dunia
kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Misri na timu yake kushika nafasi ya tatu.
Baadaye aliteuliwa kuwa nahodha wa
kikosi hicho, na baada ya miaka miwili kupita alikiongoza kikosi hicho kutwaa
ubingwa wa dunia kwa vijana na kombe la muungano wa bara la afrika na Ulaya
UEFA-CAF Meridian cup mwaka huo huo na kujumuishwa kikosi cha kwanza.
Mwezi
june 2002 katika fainali za kombe la dunia, nyota huyo alikuwa akikaa benchi na
kipa Santiago Cañizares akisimama langoni, lakini akawa
chagua namba moja baada ya kipa huyo kujitoa kikosini kutokana na majeraha.
Akiwa
na miaka 21 katika mashindano hayo aliteuliwa kuwa kipa mdogo kuliko wote.
Aliisaidia sana timu yake ya Hispania kwa
kuokoa mikwaju miwili ya penati mchezo wa hatua ya 16 dhidi ya jamhuri ya
Ireland na kupachikwa jina la “Mtakatifu”.
Na
moja kati ya hatari aliyoikoa katika mchezo wa fainali dhidi ya Korea kusini
ilichaguliwa na FIFA kuwa kati ya magoli 10 ya hatari yaliyookolewa na makipa
katika mashindano.
Ukiachana na kipa mwenzake wa Madrid
Paul wakiwa kikosi cha Hispania, kombe la mataifa ya ulaya 2008, Casillas
alipewa kitambaa cha unahodha na kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa
kundi D dhidi ya Russia na Uswizi na akapumzishwa katika kikosi kilicho mwondoa
Ugiriki na kipa Pepe Reina kusimama langoni.
Casillas aliokoa peneti mbili za
Antonia De Natale na Daniele De Rossi kwenye mchezo wa robo fainali wa Euro baina yao na Italia na walishinda penati
4-2..
Mwaka 2008 Casillas alikuwa nahodha
pekee akicheza nafasi ya golini kunyanyua kombe la mataifa ya Ulaya baada ya
Hispania kuifunga Ujerumani 1-0.
Mwaka huo huo, mlinda mlango huyo
alishika nafasi ya nne ya makipa bora zaidi katika tuzo ya Ballon d`Or nyuma ya
Cristiano Dos Santos Aveiro Ronaldo, Lionel Andrew George Messi na mchezaji
mwenzake Fernando Jose Sanz Torres.
Mwaka hu huo Casillas alitangazwa
kuwa kipa bora wa IFFHS na kupata tuzo ya mlinda mlango bora wa muda wote na
kumpiku kipa wa ujerumani Oliver Kahn.
Julai 11, 2010, akiwa nahodha wa
Hispania aliingoza timu yake kutwaa kombe la dunia lililofanyika kwa mara ya kwanza
ardhi ya afrika, nchini Afrika kusini baada ya kuitungua Uholanzi 1-0 katika
mchezo wa fainali uliofanyika dimba la kisasa la soccer city bondeni afrika
kusini.
Kwa kufanya hivyo Casillas alitangazwa
kuwa kipa wa kwanza kuongoza timu akiwa nahodha katika michuano ya kombe la
dunia mbali na makipa Gianpiero
Combi aliyefanya hivyo mwaka 1934 na Dino Zoff
mwaka 1982.
Mnamo mwaka 2011 novemba, nyota huyo
alitangazwa kuwa mchezaji mwenye mafanikio makubwa kwenye kikosi cha Hispania
akivunja rekodi ya Andoni Zubizarreta baada ya kuanza katika
kikosi
Miongoni mwa Tuzo binafsi za Iker Casillas
alizotunukiwa ni tuzo za Bravo 2000, Mchezaji bora wa mwaka wa La Liga 2000,
kuingia timu ya mwaka ya UEFA mara (6):
2007, 2008, 2009, 2010, 2011, 2012, tuzo ya Zamora 2007-8, kuingia
katika timu bora ya mashinadno ya UERO (2), 2008, 2012, kipa bora wa La Liga
(2): 2009, 2012, Mlinda mlango bora wa FIFA(5): 2008, 2009, 2010, 2011, 2012, Glove ya dhahabu ya FIFA 2010 na nyingine
nyingi.
Desemba mwaka 2012 Casillas
hakupangwa kwenye kikosi cha kwanza cha Real Madrid chini ya kocha wake Jose
Mourinho na kumpa nafasi kipa Antonia Adan, mchezo ambao klabu yake
ilikabiliana na Malaga.
Kuanzia hapo hali ya mambo kwa nyota
huyo alianza kwenda komba akiwa chini ua usimamizi wa Mourinho.
Kwa sasa kipa huyo sio chagua la
kwanza katika kikosi cha Real Madid , huku Mourinho akionekana kumwamini sana
kipa Diego Lopez ambaye amekuwa akimchezesha katika mechi za ligi na ligi ya
mabngwa barani Ulaya.
Katika hatua ya 16 ya UEFA katika
mechi mbili za Madrid dhidi ya Mnachester united, Casillas aliendelea kukaa
benchi na kuwashangaza watu wengi hata wachezaji wenzake akiwemo swahiba wake
Sergio Ramos.
Pia katika mechi za karibuni za El
Classico nyota huyo amekuwa akikosianafasi ya kuanza na kumwacha Lopez
kuendelea kutamba.
Hii inatafsiriwa na wataalamu wa
soka kuwa ni kukosekana kwa uelewano baina yake na kocha wake Jose Mourinho.
Mbali na mafanikio hayo katika soka,
lakini mchezaji huyo ni sawa na mwanadamu yeyote yule, naye ana maisha yake nje
ya uwanja.
Tanga mwaka 2009 Casillas amekuwa
katika mahusiano ya kimapenzi na mwandishi wa habari za michezo Sar Carbonero.
Wawili hawa wametajwa kupendana sana
na kutumia muda wao mwingi kujadili mambo yao ya maisha wanapokuwa nje ya kazi
zao.
Juhudi za Casillas katika mazoezi na
kuipenda kazi yake ya soka ndio siri ya mafanikio yake katika soka na hii
inawafundisha wachezaji wa Kitanzania kuzingatia nidhamu ya kazi yao na
kujituma katika mazoezi.
0 comments:
Post a Comment