VIJANA WA SIMBA |
Na Baraka
Mpenja
Mabingwa
watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, wekundu wa Msimbazi Simba “Taifa Kubwa”
baada ya jana kukabwa koo kwa kutoa sare ya 2-2 na vijana wa mitaa ya
Kishamapanda jijini Mwanza, Toto Afrika,uwanja wa CCM-Kirumba, leo wameshuka
dimbani mkoani Shinyanga kumenyana na Shinyanga United mechi ya kirafiki.
Dakika
tisini za mchezo huo wenye lengo la kuwapa uzoefu zaidi makinda wake ambao
Simba inawatumia kwa mechi zilizosalia kipute cha ligi kuu ilimalizika kwa sare ya 1-1 katika uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga huku bao la Simba likifungwa Ramadhani Kipalamoto.
Simba
wapo katika safari ya kusuka upya kikosi
chake ambacho kimesheeni vijana na kuwatupa wakongwe kadhaa “Mafaza” kwa sababu
ya kukosa nidhamu katika kazi yao inayowapa kipato.
Miongoni
mwa wachezaji waliotemwa ni kiungo Haruna Moshi `Boban`, Ramadhan Chombo `Redondo`, Mwinyi kazimoto
Mitula, washambuliaji ni Abdallah Juma na Mzambia Ferlix Mumba Sunzu; mabeki Juma Said Nyosso, Amir Maftah, Komabil Keita, na Paul Ngalema.
Kabla
ya kwenda Mwanza kucheza na toto, Simba alitokea Kaitaba kucheza na Kagera
sugar huku ikiwa imepita mkoa ya Singida na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya
Singida united huku ikishinda 4-0 na baadaye ilisafiri mpaka mkoani Tabora kupigishana
madaluga na maafande wa Rhino Rangers waliokata tiketi ya kushiriki kipute cha
ligi kuu bara msimu ujao, mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1.
Kwa
mjibu wa Afisa habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga maarufu kwa jina la Mr.
Liverpool amekaririwa akisema sasa ni wakati wa mashabiki na wanachama wa klabu
hiyo kutulia kwani benchi la ufundi likiongozwa na kocha Mfaransa Patrick
Liewig, linafumua kikosi na kuunda timu mpya ya ushindani msimu ujao.
Kamwaga
amesema katika mchezo wa leo mkaoni Shinyanga vijana wameonekana kuimarika sana
huku wakicheza kwa kujiamini kama jana walivyofanya CCM kirumba licha ya
kuambulia sare.
Simba
ambao ni mabinwa watetezi wa taji, wanaonekana kuweka rehani ubingwa wao na
kuziachia klabu za Azam fc yenye pointi 43 na Vianara Yanga wenye pointi 49
kuchuana vikali kuwania mwari wa ligi kuu msimu huu.
Matokeo
ya jana dhidi ya Toto, yamemfanya Mnyama pori, Simba ashuke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu
kwa pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 21, nyuma ya Kagera Sugar yenye
pointi 37.
0 comments:
Post a Comment