Na Baraka Adson
Wapenzi, wanachama na viongozi wa mabingwa wa kandanda Tanzania bara, wekundu wa msimbazi simba wameaswa kuwa na utulivu wakati huu wa mpito klabuni hapo ili kuepuka migogoro ambayo itaitafuna na kuimaliza klabu bila sababu ya msingi.
Wakizungumza na MATUKIO DUNIANI kwa nyakati tofauti makocha John Wiliam "Del Piero" anayekinoa kikosi cha mabingwa wa zamani wa Tanzania klabu ya African Sports ya Tanga na mjumbe wa kamati ya ufundi ya Simba pamoja na kocha wa zamani wa Yanga Keny Mwaisabula "Mzazi" wametoa wito huo kwa wana simba wote baada ya kutolewa ligi ya mabingwa barani afica kwa kufungwa 1-0 nyumbani na 4-0 ugenini na Libolo ya Angola.
Piero kwa upande wake alisema simba ya sasa inahitaji kujipanga upya kwa ajli ya ligi kuu Tanzania bara na michuano ya kimataifa mwakani kwani kwa sasa haina wachezaji wazuri tofauti na msimu uliopita.
"Simba kwa sasa imekosa huduma ya Kelvin Patrick Philip Yondan anayekiga Yanga, Emmanuel Anold Okwi ambaye yupo Tunisia, Patrick mutesa Mafisango ambaye ni marehemu, mungu ailaze roho yake mahali pema peponi na wengine ambao walikuwa muhimu sana. kwa kikosi cha sasa kinahitaji kupewa muda na kubadilishwa ili kupata mafanikio" Piero alisema.
Kocha huyo aliongeza kuwa magoli mengi ya simba yanatokana na makosa ya mabeki wake ambao wanashindwa kukaba kwa uangalifu na kuwaruhusu wapinzani wao kufunga kirahisi.
Piero alishauri kuwa kipigo cha 4-0 kutoka kwa Libolo kisiwe kigezo cha vurugu Msimbazi, bali ni wakati kwa wapenzi wa simba kuwa na mshikamano mkubwa ili kushirikiana na benchi la ufundi linaloongozwa ma makocha watatu, Mfaransa Patrick Liewig, Mganda Moses Basena na Mzalendo Jamhuri Khwelu Julio.
"Binafsi sio mwumini wa vurugu, napenda utulivu na amani, wanasimba wote tunahitaji kuwa makini na wachochezi ambao hawana mapenzi mema na simba ili tuijenge timu yetu kwa uzuri" Piero alionya.
Kwa upande wake Kocha Mwaisabula "mzazi" alisema Libolo waliwazidi Simba kwa kila idara na ndio maana waliwafunga kirahisi nyumbani na ugenini.
Mwaisabula alisema Libolo walitumia gharama nyingi kutafuta ushindi ugenini kwa kutuma viongozi wao kuiangalia Simba, hii inaonesha jinsi gani wapo makini na wanajitambua.
"Wenzetu wanatumia zaidi ya milioni 120 kuandaa mazingira ya ushindi wa mechi moja, sisi tunaandaa timu kwa kambi inayogharimu milioni 20 hadi 30, hatutaweza kufanya vizuri hata kidogo". Mwaisabula aliongeza.
Pia kocha huyo aliwata wana simba kutulia na kuacha maneno ya kuiponda klabu yao kwa madai ya kufanya vibaya ligi kuu na ligi ya mabingwa barani afrika.
"simba ipo nafasi ya tatu kati ya timu 14 za ligi kuu, mtu anaposema imefanya vibaya, binafsi sielewi ana maana gani, kama simba haifanyi vibaya kwa kuwa nafasi hiyo, je African Lyon wanafanyaje?, hakika mashabiki wa simba watulie". Mwaisabula alishauri.
Home
»
»Unlabelled
» WANA SIMBA WATAKIWA KUTULIA KIPINDI HIKI CHA MPITO KLABUNI HAPO
Tuesday, March 5, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment