Thursday, March 7, 2013

 
KIKOSI kizima cha Azam FC leo kinaingia kambini katika hosteli za Azam Complex, zilizopo Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Barrack Young Controllers II ya Liberia.
Azam iliyoitoa Al Nasir Juba ya Sudan Kusini katika Raundi ya kwanza, kwa jumla ya mabao 8-1, itamenyana na Barrack Young Controllers II kati ya Machi 15 na 17 mwaka huu katika mchezo wa kwanza Liberia kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye, Dar es Salaam.
Akizungumza mchana wa leo, Katibu wa Azam, Nassor Idrisa alisema kwamba wanamshukuru Mungu kwa mafanikio ya awali na sasa wanajipanga kwa mtihani ulio mbele yao, ambao ndio mgumu zaidi.
Alisema mafanikio ya awali ya Azam ni maandalizi ya muda mrefu na sasa kilichobaki ni muendelezo wa programu hiyo ya maandalizi.
Nassor alisema kwamba wanaomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lisogeze mbele mechi zao mbili za wiki ijayo ili wapate dursa ya kujiandaa vema na mechi ya Barrack Young Controllers II.
“Jumatano (wiki ijayo) ndiyo siku ambayo tunatarajia kuondoka hapa kwenda Liberia, na ukiangalia kwenye ratiba ya Ligi Kuu tutakuwa tuna mechi na Jumamosi ambayo tutakuwa tayari Liberia, pia tumepangiwa kucheza,”.
“Sasa tunaiomba TFF itusogezee mbele mechi hizi mbili ili tupate fursa nzuri ya kujipanga kwa mtihani huu wa kuiwakilisha nchi,”alisema Nassor.
Kuhusu afya za wachezaji, Nassor alisema majeruhi kwa sasa ni mmoja tu Samih Hajji Nuhu, lakini wengine wote wapo fiti na wameingia kambini leo.
Aidha, Nassor aliwataja wachezaji wanaoombewa viza kwa safari ya Liberia kuwa kuwa ni makipa; Mwadini Ally na Aishi Manula, mabeki; Joackins Atudo (Kenya), David Mwantika, Himid Mao, Malika Ndeule, Waziri Salum na Luckson Kakolaki.
Kwa upende wa viungo ni Abdulhalim Humud, Kipre Balou (Ivory Coast), Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Salum Abubakar, Humphrey Mieno (Kenya), Abdi Kassim ‘Babbi’, Uhuru Suleiman na Khamis Mcha ‘Vialli’ wakati washambuliaji ni John Bocco ‘Adebayor’, Kipre Tchetche (Ivory Coast), Seif Abdallah, Brian Umony (Uganda) na Gaudence Mwaikimba. 
Aliwataja wachezaji watatatu watakaoachwa kuwa ni kipa Jackson Wandwi na mabeki Omar Mtaki na Samih Hajji Nuhu.
Kama ilivyotarajiwa na wengi, Azam ndio timu pekee iliyobaki kwenye michuano ya Afrika, baada ya mwishoni mwa wiki kuitoa Al Nasir ya Juba.
Katika mchezo huo, mabao ya Azam yalifungwa na Khamis Mcha ‘Vialli’ matatu, John Raphael Bocco na Salum Abubakar ‘Surer Boy, moja kila mmoja.
Jamhuri ya Pemba, ilikuwa timu ya kwanza ya Tanzania kuaga michuano ya Afrika, baada ya Jumapili kufungwa mabao 5-0 na wenyeji Kedus Giorgis nchini Ethiopia katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.
Matokeo hayo, yanamaanisha, Jamhuri imeaga kwa kufungwa jumla ya mabao 8-0, baada ya awali kutandikwa 3-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Gombani, Pemba.
Wawakilishi wengine wa Bara katika michuano hiyo, Simba SC wametolewa pia baada ya kufungwa mabao 4-0 na Recreativo de Libolo ya Angola kwenye Uwanja wa Manispaa mjini Calulo, Angola.
Matokeo hayo, yanaifanya Simba itolewe kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya awali kufungwa bao 1-0 Dar es Salaam. Viva Azam.

kutoka Bin Zubeiry

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video