Sunday, March 10, 2013

KIKOSI CHA WAZEE WA KAZI, TANZANIA PRISONS YA JIJINI MBEYA

Na Baraka Adson
Maafande wa Tanzania Prisons kesho asubuhi wanaanza kambi Ukonga jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara wiki ijayo dhidi ya wana lambalamba Azam fc.

Sadick Jumbe, katibu mkuu wa klabu hiyo ameiambia MATUKIO DUNIANI kuwa  kikosi kizima kipo salama  kuanza mazoezi yao chini ya kocha mkuu Jumanne Chale.

Jumbe aliongeza kuwa wanakwenda kukabiliana na Azam ambayo watakosa huduma ya beki wake David Mwantika aliyetokea klabu hiyo yenye makazi yake jijini mbeya baada ya  jana kulimwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi kuu  dhidi ya Polisi Morogoro uliochezwa Chamazi na timu hizo kutoka sare ya 1-1.

"Mchezo dhidi ya Azam ni mgumu sana, nyumbani tulitoka nao suluhu, jana tumewaona wakicheza na Polisi, ni wazuri sana, inatupa wakati mgumu wa kujiandaa ili kupata matokeo ". Jumbe alisema.

Akimzungumzia mshambuliaji wao Emmanuel Gabriel mwakyusa, Jumbe amesema nyota huyo amekaa muda mrefu bila kucheza na ndio maana kwa sasa hana makali.

Alisema anahitaji muda kwa sasa ili kurejesha makali yake na kocha mkuu Chale anampa mazoezi mazuri ya kurudisha mechi "fitiness".

Pia alisema wamebakiza mechi tatu nyumbani, watajitahidi kuzitumia vizuri ili kujinusuru kushuka daraja ingawa rekodi zao ni mbaya katika uwanja wao kwani tangu ligi ianze mzunguko wa kwanza na sasa wa pili  wameshinda mechi mbili tu, walishinda dhidi ya Toto Africans 1-0 na Africa Lyon 2-0.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video