>>NANI KUTINGA ROBO FAINALI??
MECHI za Marudiano za UCL, UEFA
CHAMPIONZ LIGI, zinaendelea leo kwa Mechi mbili kati ya Juventus na
Celtic huku Juve wakiongoza kwa Bao 3-0 toka Mechi ya Kwanzawaliyoshinda
ugenini na Paris St Germain kurudiana na Valencia waliyoifunga Bao 2-1
ugenini.
+++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
-Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku
-Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Jumatano 6 Machi 2013
Juventus v Celtic [3-0]
Paris St Germain v Valencia [2-1]
+++++++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
PARIS SAINT-GERMAIN FC V VALENCIA CF (2-1)
PSG wamewahi kushinda Mechi zao zote 13
za Mashindano ya UEFA baada ya kupata ushindi wa ugenini katika Mechi ya
kwanza lakini hii ni mara ya kwanza kwao kutinga Raundi ya Mtoano tangu
Mwaka 1994/95 ambako walikomea Nusu Fainali.
Kipigo cha Valencia cha 2-1 mikononi mwa
PSG katika Mechi ya kwanza kimevunja ile Rekodi ya Valencia ya
kutofungwa na Klabu za France katika Mechi 17.
Hata hivyo, Valencia hadi sasa
hawajafungwa na Klabu yeyote ya France katika Mechi 8 walizocheza Nchini
France ambazo wameshinda 4 na sare 4.
JUVENTUS V CELTIC FC (3-0)
Juventus hawajafungwa kwenye Mashindano
ya Klabu Barani Ulaya tangu Tarehe 18 Machi 2010 walipochapwa Bao 4-1
Uwanjani Craven Cottage na Fulham kwenye UEAF EUROPA LIGI na ubwagwa nje
kwa Jumla ya Bao 5-4 kwa Mechi mbili.
Baada ya hapo, Juventus, katika Mechi za
Ulaya, wameshinda Mechi 8 na sare 9 huku wakishinda Mechi zao 4
zilizopita bila kufungwa hata Bao moja.
Celtic, wakicheza Raundi hii kwa mara ya
kwanza katika Misimu mitano, hawajawahi kushinda hata mara moja katika
Mechi zao 9 walizocheza Italy.
Katika Mechi zao 20 na Klabu za Italy
Matokeo ni Ushindi 5, Sare 7 na Kufungwa 8 huku zile zilizochezwa Nchini
Italy zikiwa Ushindi 0, Sare 3 na Kufungwa 9.
Kumbukumbu kubwa ya Celtic ni ya yale
Mashindano yao ya kwanza Barani Ulaya ambapo walifanikiwa kuwa Klabu ya
kwanza toka Uingereza kutwaa Kombe la Ulaya kwa kuichapa Inter Milan Bao
2-1 kwenye Fainali huko Lisbon, Ureno Mwaka 1966/67.
UCL: RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
RATIBA:
-Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku
-Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Jumanne 12 Machi 2013
Barcelona v AC Milan
Schalke v Galatasaray
Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal
Malaga v FC Porto
+++++++++++++++++++++++++++
ROBO FAINALI:
Mechi ya 1=Tarehe 2 na 3 Aprili 2013
Mechi ya 2= Tarehe 9 na 10 Aprili 2013
NUSU FAINALI
Mechi ya 1= Tarehe 23 na 24 Aprili 2013
Mechi ya 2= Tarehe 30 Aprili na 1 Mei 2013
FAINALI
25 Mei 2013
UWANJA wa WEMBLEY, London.
kutoka soka in Bongo Leo
0 comments:
Post a Comment