Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), SteveKilindo
(katikati), akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Ibrahim
Msengi msaada wa magodoro kwa ajili ya Hosptali ya Huruma ya wilayani
Rombo pamoja na Kituo cha Afya cha Uru Kiaseni katika hafla iliyofanyika
Mjini Moshi. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako.
Jumla ya magodoro 210 na vyandarua 200 vimetolewa na TBL kwa ajili ya
kituo hicho na hospitali hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Dk. Ibrahim Msengi akikabidhi msaada wa magodoro kwa Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Mtumwa Mwako baada ya kukabidhiwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), mjini Moshi . Katikati ni Mkurugenzi wa
Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo. Jumla ya magodoro 210 na
vyandarua 200 vimlitolewa na TBL kwa ajili ya kituo Afya cha Uru Kiaseni
na Hosptali ya Uhuruma .
Mkurugenzi wa Uhusiano na
Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL, Steve
Kilindo,(katikati)wakifurahia jambo na kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Dk Ibrahm Msengi (Kulia )pamoja na mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Dk Mtumwa Mwako mara baada yaTBL kukabidhi msaada wa magodoro 210 na
vyandarua 200 kwa kituo cha Afya cha Uru Kiaseni na hosptali ya Uhuruma .
Magodoro yaliyokabidhiwa na TBL kwa Hospitali mkoani Kilimanjaro
………………………………………………………………………..
WADHAMINI wakuu wa mbio za
Kilimanjaro Marathon, kampuni ya Bia ya TBL, imekabidhi msaada wa
magodoro na vyandarua kwa uongozi wa hosptali ya Huruma na kituo cha
Afya cha Uru Kiaseni kama sehemu yamaandalizi ya mbio za Kilimanjaro
marathon zinatarajia kufanyika leo machi
3.
Misaada ya aina hiyo hufanywa
kila mwaka na TBL wakati wa maandalizi ya Mbio za Kilimanjaro Marathon
ambazo hufanyika kila mwaka ikiwa ni utaratibu wa kampuni hiyo kurudisha
faida iliyopatikana kwa wananchi kutokana na utumiaji wa bidhaa zake.
Akizungumza katika hafla ya
makabidhiano, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo,
alisema kuwa TBL imeamua kufanyautaratibu huo ambao wamekuwa wakifanya
kila mwaka na mwaka huu
wameonelea ni vyema wakatoa msaada katika hospitali hizo.
Kilindo alisema kuwa msaada wa magodoro hayo 210 na vyandarua 200 ni
jitihada za kampuni hiyo kuhakikisa jamii ya Tanzania inafurahi na
kujivunia kilicho chao na kuongeza kuwa hicho wal;ichokitoa ni sehemu
ya shukuruni kwa watanzania ambao wamekuwa wakiwaunga mkono kila mara.
“Kama wadhamini wakuu wa mbio
hizi, tumekuwa tukishiriki katika shughuli nyingi za kijamii na moja yao
ni kutoa msaada katika mahospitali, leo tunatoa magodoro 210 na
vyandarua 200 kwa hospitali
za Kiaseni ya Rau na Huruma ya Rombo, tunaamini katika hili tutakuwa
tuimesaidia kwa kiasi fulani,” alisema Kilindi
Naye Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Ibrahimu Msengi akipokea
msaada huo kwa niaba ya uongozi wa hospitali hizo aliipongeza TBL kwa
kuamua kuijali jamii inayonunua na kutumia bidhaa zao na kuongeza kuwa
msaada huo anaamini utakuwa wa manufaa makubwa kwa wagonjwa katika
hospitali hizo.
“Moyo wa kutoa sio lazima uwe
nacho, TBL wameonesha kuwa kazi yao sio kutengeneza bia tu, bali
wanaweza kujali jamii na katika hili nawapongeza sana na ningependa
mashirika na makampuni mengine nayoyangekuwa yanafanya hivi,” alisema
Msengi.
Msengi alitoa wito kwa
wafanyabiashara wote na wamiliki wa makampuni kuiga mfano mzuri
ulioonesha na TBl na kusisitiza umuhimu wa kutoa kwani jukumu la
kuhudumia jamii ni la kila mtu na sio serikali pekee.
Kuhusu mbio za mwaka huu za
Kilimanjaro marathon Dkt. Msengi alisema,mbio hizo kufanyika katika
ardhi ya Kilimanjaro ni fahari na kuongeza kuwa matarajio ya wote ni
kuona kila mtu akinufaika na mbio hizo huku
akiwatakia kila kheri wakimbiaji wote hasa wakimbiaji wa Tanzania.
“Nitumie Fursa hii kuwatakia
kila la Kheri wakimbiaji wote wa Kilimanjaro marathon, kila la kheri
watanzania wote watakaotuwakilisha keshokutwa naamini tutashinda,”
alisema.
Kwa upande wake Mganga mnku wa mkoa wa Kilimanjaro (RMO), Dk. Mtumwa
Mwako, akipokea magodoro na vyandarua hivyo kutoka kwa kaimu mkuu wa
mkoa kwa niaba ya uongozi wa
Hospitali za Kiaseni na Huruma, alisema kuwa msaada huo utasaidia
kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa mama na mtoto.
Nao madaktari kutoka katika
hospitali hizo, Dkt. Godwin Kiwelu wa hospitali ya Huruma ya Rombo na
Dk. Delfina Materu wa hospitali ya Kiaseni ya Rau, walisema kwa msaada
huo mzigo wa changamoto
zinazokabili hospitali hizo
zimepungua huku wakisisitiza kuwa bad kuna changamoto nyngi ambazo
inatakiwa jamii inatakiwa kujitokeza kusaidia kama walivyofanya TBL.
0 comments:
Post a Comment