Homa ya pambano la kuwania kufuzu kombe la dunia kwa mwaka
2014 nchini Brazil baina ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars inayonolewa
na kocha Mdenish Kim Paulsen dhidi ya miamba ya soka kutoka kaskazini mwa
afrika, timu ya taifa ya Morroco, simba wa milima ya Atlas inazidi kupanda huku
wadau wa soka wakiendelea kutuma salama za kuitakia ushindi stars katika mchezo
huo utakaopigwa siku ya kesho kuanzia saa 9 alasiri.
Abdallah King Kibaden, kocha mkuu wa Kagera sugar inayocheza
ligi ya premia Tanzania bara na mchezaji wa zamani wa stars amewaombea kila la
heri wachezaji wa stars ili wapate matokeo mazuri ya uwanjani.
Kibaden amesema Morroco ni timu nzuri lakini wachezaji wetu
kwa sasa ni wazuri, kikubwa ni dua za watanzania na kujitokeza kwa wingi kesho
dimba la taifa Dar es salaam.
Merck Mexme, nahodha wa Zamani wa taifa stars na kocha mkuu
wa vijana wa manungu, Mtibwa sukari, naye kwa upande wake amesema vijana wa
stars kwa sasa wanapata mechi nyingi za kirafiki hivyo imani yake kubwa ni
kupata ushindi mchezo wa kesho katika dimba la nyumbani.
Mexeme amesema Morroco si timu ya kubeza , cha msingi ni
vijana kuwa makini kwani timu hiyo kutumia wachezaji wengi wa ndani ni hatari
zaidi.
Morroco amesema mchezo wan kesho ni mgumu sana, cha msingi
wachezaji wafanye kazi kubwa ili kupata matokeo mazuri.
Pia amesema wachezaji wa morocco ni wazuri, hivyo kama
watapata goli la kuongoza watanzania wasije kukata tama kuishangilia timu.
0 comments:
Post a Comment