Monday, March 11, 2013


KATIBU wa Simba SC, Evodius Mtawala amesema kwamba matatizo ya madeni yanayoisumbua klabu kwa sasa, yanatokana pia na klabu hiyo kutolipwa na wadai wake, hivyo kushindwa kulipa madeni.

Akizungumza mida hii, Mtawala alisema Simba SC inadai zaidi ya Sh. Milioni 500, wakati yenyewe madeni yake hayafiki hata Sh. Milioni 100.
Alisema Push Mobile pekee wanaidai zaidi ya Sh. Milioni 50, wakati klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia wanaidai zaidi ya Sh. Milioni 450 kutokana na mauzo ya mshambuliaji Emmanuel Okwi. 
“Etoile hawataki kulipa, hadi sasa imebidi tuanze kuwasiliana na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) kufanya mpango wa kumrudisha mchezaji wetu,”amesema Mtawala.
Mtawala amesema kwa sasa wapo katika mchakato wa kuwapangia nyumba makocha na wachezaji wa kigeni wa timu hiyo na tayari kocha Mkuu, Patrick Liewig amepatiwa nyumba maeneo ya Kunduchi.
Kuhusu madai ya mishahara ya kocha huyo, Mtawala amesema anadai mshahara wa mwezi Februari tu, kwani mshahara wake wa kwanza wa Januari alilipwa na mwezi wa tatu haujaisha.
“Kwa sasa tunapambana na Push Mobile waweze kutulipa ili tulipe madeni ya Sapphire Court Hotel na Spice. Kuendesha timu ni gharama kubwa, na sisi kwa sasa timu yetu haifanyi vizuri mashabiki hawaji uwanjani, hatupati fedha,”alisema Mtawala.
Mtawala amesema ni kweli Simba SC kuna matatizo kwa sasa, lakini ametahadharisha watu wasiyakuze.
Jana usiku Meneja wa Simba SC, Moses Basena, kipa Abbel Dhaira na kiungo Mussa Mudde, wote raia wa Uganda, walifukuzwa kwenye hoteli ya Spice, Kariakoo, Dar es Salaam kutokana na klabu hiyo kulimbikiza deni la Sh. Milioni 27.
Pamoja na kufukuzwa kwa Waganda hao usiku huo, uongozi wa Spice Hotel unashikilia magari mawili ya Simba SC, basi dogo na gari la kocha, aina ya GX110 hadi ulipwe fedha zake.
Kutokana na kufukuzwa Spice, Waganda hao walikwenda kuomba hifadhi katika hoteli ya Sapphire, ambako walipokelewa na kupewa vyumba vitatu. Kocha Mfaransa, Patrick Liewig pekee ameachwa aendelee kuishi katika hoteli ya Spice. 
Mapema jana mchana, uongozi wa hoteli ya Sapphire Court, iliyopo Kariakoo pia, uliwazuia hotelini wachezaji wa Simba SC waliokuwa kambini hotelini hapo, ukishinikiza kulipwa deni la Sh. Milioni 25.7.
Simba SC ilizuiwa ikiwa inajiandaa kwenda Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hata hivyo, baadaye kaimu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itangare ‘Kinesi’ alikwenda kuzungumza na wamiliki wa hoteli hiyo na kufikia mwafaka wa kulipa baada ya mechi ya Coastal.
Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala amesaini hati ya kuahidi kulipa deni hilo baada ya mechi na Coastal. 
Hamkani si shwari sasa ndani ya Simba SC, kufuatia viongozi wawili wa Kamati ya Utendaji, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Zacharia Hans Poppe kujiuzulu wiki iliyopita.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage yuko India kwa matibabu na Kinesi aliyeteuliwa kukaimu Umakamu Mwenyekiti, sasa ndiye anakaimu Uenyekiti wa klabu.
Aidha, Baraza la Wazee kwa pamoja na Baraza la Wadhamini, wameunda Kamati Maalum ya kusimamia timu kuhakikisha inafanya vizuri katika wakati huu mgumu, chini ya Mwenyekiti, Rahma Al Kharoos, maarufu kama Malkia wa Nyuki.
Malkia wa Nyuki alianza vyema jana baada ya kuiongoza Simba SC kuilaza 2-1 Coastal Union.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video