Na Baraka Adson
Pambano kali la kukata na shoka la kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazili baina ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars dhidi ya simba wa milima ya Atlas, timu ya taifa ya Morroco ndani ya uwanja wa taifa wa Dar es salaam limemalizika kwa stars kuibuka kifua mbele kwa ushindi mnono wa mabao 3-1.
Mabao yote ya stars yamefungwa kipindi cha pili, mabao hayo yametiwa kambani na Thomas Ulimwengu aliyefunga moja na Mbwana Ally Samata akitia kambani mawili.
MBWANA SAMATA ALIYEFUNGA MABAO MAWILI JIONI HII |
THOMAS ULIMWENGU |
Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua , vijana wa Taifa stars wameonesha kandanda la ajabu na kuonesha kuwa, " ukitaka kuona mbio za kinyonga choma moto kichaka".
Stars ambao hawana jina kubwa ukilinganisha na Morroco waliwapoteza kabisa Morroco walioanza kipindi cha kwanza kwa kupiga mashuti kadhaa langoni mwa stars lakini mlinda mlango namba moja wa stars TANZANIA ONE Juma Kaseja akiokoa kwa umahiri mkubwa.
Wachezaji wa stars kama Amri Athman Kiemba, Mrisho Ngasa, Mbwan Samata, Mwinyi kazimoto, Sure boy, Frank Domayo, Thomas Ulimwengu wamecheza soka la kuvutia na kuibua shangwe kubwa kwa mashabiki wa soka waliofika uwanjani.
Pia wachezaji Erasto Edward Nyoni na Agrey Morris ambao hawana timu kwa sasa walizua maneno baada ya kocha mkuu wa stars Kim Paulsen kuwaamini na kuwajumuisha katika kikosi chake, leo hii wamewadhihirishia watanzania kuwa wanaweza kucheza soka baada ya kuonesha kiwango cha juu wakiwa safu ya Ulinzi ya stars.
Katika Mechi hiyo ya Ivory Coast na Gambia, Ivory Coast walifunga Bao zao zote Kipindi cha Pili kupitia Bony Wilfred, kwa Penati ya Dakika ya 49, Yaya Toure, Dakika ya 59 na Salomon Kalou, Dakika ya 70.
KUNDI
C
1
Côte d'Ivoire Mechi 3 Pointi 7
2
Tanzania Mechi 2 Pointi 6
3
Morocco Mechi 2 Pointi 2
4
Gambia Mechi 3 Pointi 1
0 comments:
Post a Comment