Wednesday, March 13, 2013

KIKOSI CHA MAAFANDE WA RUVU SHOOTING KUTOKA MKOANI PWANI

Na Baraka Adson
Maafande wa Jeshi la kujenga taifa kutoka mkoani Pwani, klabu ya Ruvu shooting imetoa onyo kali kwa waamuzi watakaochezesha mchezo wao wa mach 16 jumamosi wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya klabu ya Yanga ya Dar es salaam katika uwanja wa taifa kuwa makini zaidi na kuchezesha kwa haki.

Afisa habari wa klabu hiyo, Masau Bwire "Mzee wa Tambo" amesema wao hawaogopi wazee wa Uturuki na siku hiyo watawaonyesha cha mtema kuni na kuwaduwaza watanzania wanaoamini kuwa soka la Bongo ni Simba na Yanga tu.

"Wanawaita wazee wa Uturuki, tutawageuza jina hilo na watashangaa jinsi vijana wa Charles Boniface Mkwasa wanavyopiga soka safi na kupata matokeo mazuri ya uwanjani endapo waamuzi watachezesha kiungwana na kuepuka kuwapa mbeleko wapinzani wetu". Masau alisema.

Aidha Masau alisema vijana wana morali kubwa na wamekamilika kwa kila kitu na Yanga wanawafahamu vizuri Ruvu shooting ambao ni moto kwao kila wanapokutana.

Masau aliongeza kuwa soka kama unalijua utacheza tu, hakuna haja ya kwenda uingereza wala uturuki, wao walibaki hapa na wanataka kuonesha kuwa wanaweza sana.

Pia Masau alisisitiza kuwa wamebakiwa na mechi nane kwa sasa na wanahitaji kufanya vizuri wakianza kuwashughulikia Yanga jumamosi, halafu watafuata Azam fc na wengine.

MCHEZAJI WA RUVU SHOOTING KULIA AKIMILIKI MPIRA MBELE YA MCHEZAJI WA YANGA KWENYE KATI YA MECHI WALIZOKUTANA


kwa upande wa wenyeji wao, klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, kupitia kwa afisa habari wake Baraka Kizuguto wamesema wao wanasimamia kauli mbiu yao ya kushinda mechi zote tangu watoke Uturuki walipoweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na ngwe ya lala salama ya ligi kuu Tanzania bara.

Kizuguto alisema Ruvu shooting ni timu nzuri lakini wanajiandaa vizuri ili kuwabamiza na kuendelea kujikita kileleni wakiongoza wakiwa na alama 45 kibindoni nyuma ya Azam fc wenye alama 36, huku mnyama Simba mwenye alama 34 kibindoni akiwa katika nafasi ya tatu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video