RUVU SHOOTING |
Na Baraka Mpeja
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika
michuano ya kimataifa barani Afrika, klabu ya Azam fc wamesafiri mpaka Mabatini
Mlandizi Mkoani Pwani kuwafuata maafande watutkutu wa jeshi la kujenga taifa,
klabu ya Ruvu shooting ya mkoani humo kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania
bara hapo kesho.
Akizungumza
leo hii, afisa habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd Maganga, amesema kuwa
mchezo huo utakuwa mgumu sana kwao na
wanauchukulia kwa umakini mkubwa sana ili kupata pointi tatu muhimu katika
harakati zao za kuwania ubingwa msimu huu.
Idd
alisema mchezo huo watautumia kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano wa
kombe la shirikisho dhidi ya Waliberia, Barrack Fc wiki ijayo katika dimba la
taifa jijini Dar es salaam.
“Sisi
kila mchezo kwetu ni fainali, katu hatudharau timu yoyote ya ligi kuu, mchezo
wa kesho ni mgumu sana , Ruvu shooting ni wazuri sana, lakini tutapambana
dakika zote ili kutwaa pointi tatu baadaye tutarudisha akili zetu kombe la
shirikisho”. Idd alisema.
Pia
afisa habari huyo aliongeza kuwa Azam fc watashusha kikosi kizima Mabatini na
mapaka sasa hawana majeruhi yeyote anayeweza kuukosa mchezo huo muhimu.
Kikubwa
Idd amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutulia na kuwaunga mkono wakati huu
muhimu wa kuwania taji la ligi kuu na kombe la shirikisho barani Afrika.
Azam
fc wapo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 40 huku
Yanga wakiwa kileleni na pointi 48. Mabingwa watetezi Simba wapo nafasi ya tatu na pointi 34 baada ya kupoteza
1-0 mchezo uliopita dhidi ya Kagera
sugar.
Ligi
kuu kwa sasa imejigawa katika makundi matatu, kundi la kwanza ni timu
zinazowania ubingwa wa ligi kuu kwa maana ya Yanga, Simba na Azam fc, kundi la
pili ni zle zinazowania nafasi mojawapo za juu, Mtibwa Sugar, Coastal union,
kagera sugar, JKT Oljoro, Ruvu shooting na kundi la mwisho ni zile zinazowania
kukwepa mkasi wa kushuka daraja, JKT Ruvu, Tanzania Prisons, Toto Africans,
African Lyon.
Kwa
upande wa Ruvu Shooting wamesema wapo tayari kuwachinja Azam fc kutokana na
maandalizi makubwa waliyowafanya chini ya kocha Mzalendo, Charles Boniface
Mkwasa “Master”.
Akizungumza
na mtandao huu, Afisa habari wa Ruvu shooting, Masau Bwire, amesema kuwa
maandalizi ya mchezo huo yanakwenda swadakita kabisa huku kazi kubwa ya Mkwasa
ni kurekebisha makosa yaliyojitokeza mchezo uliopita ambao walifungwa 1-0 na
vinara wa ligi hiyo, klabu ya Yanga.
“Wapinzani wetu wamefanya vizuri kombe la
shirikisho kwa kuwafunga Barrack Young Controller II mabao 2-1 ugenini, pia
walipata matokeo mazuri mbele ya Prisons na sasa wamepata nguvu ya kusaka mwari
wa ligi kuu, sisi tunahitaji nafasi ya kushiriki hata Tusker cup mwaka huu,
hatukubali kufungwa”. Masau alitamba.
“Watanzania wanatujua vizuri Ruvu shooting,
moto tunaowasha si mchezo, tutawapiga Azam fc na baada ya hapo tutaanza hesabu
za kuwavaa Polisi Morogoro wiki ijayo”. Masau aliongeza.
Hapo
chini ni Ratiba na Msimamo wa ligi kuu Tanzania bara kabla ya mitanange ya
kesho.
JUMAMOSI MACHI 30
JKT OLJORO v JKT RUVU [SH. AMRI ABEID,
ARUSHA]
RUVU SHOOTINGS v AZAM FC [MABATINI, PWANI]
AFRICAN LYON FC v COASTAL UNION [AZAM
COMPLEX, KAGERA]
POLISI MOROGORO v YOUNG AFRICANS [JAMHURI,
MOROGORO]
KAGERA SUGAR v MTIBWA SUGAR FC [KAITABA,
KAGERA]
TOTO AFRICANS v SIMBA SC [CCM KIRUMBA,
MWANZA]
MSIMAMO:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GD
|
PTS
|
1
|
YANGA
|
20
|
15
|
3
|
2
|
25
|
48
|
2
|
AZAM FC
|
20
|
12
|
4
|
4
|
19
|
40
|
3
|
SIMBA
|
20
|
9
|
7
|
4
|
11
|
34
|
4
|
KAGERA
|
21
|
9
|
7
|
5
|
5
|
34
|
5
|
COASTAL
|
21
|
8
|
8
|
5
|
4
|
32
|
6
|
MTIBWA
|
21
|
8
|
8
|
5
|
4
|
32
|
7
|
RUVU SHOOTING
|
19
|
8
|
5
|
6
|
3
|
29
|
8
|
JKT OLJORO
|
21
|
6
|
7
|
8
|
-3
|
25
|
9
|
MGAMBO
|
21
|
7
|
3
|
11
|
-6
|
24
|
10
|
PRISONS
|
21
|
4
|
8
|
9
|
-9
|
20
|
11
|
JKT RUVU
|
18
|
5
|
4
|
9
|
-12
|
19
|
12
|
POLISI
|
21
|
3
|
8
|
10
|
-10
|
17
|
13
|
TOTO
|
21
|
3
|
8
|
10
|
-12
|
17
|
14
|
LYON
|
21
|
4
|
4
|
13
|
-18
|
16
|
0 comments:
Post a Comment