Thursday, March 14, 2013

KIKOSI CHA MAAFANDE WA TANZANIA PRISONS, "WAJELA JELA" KWENYE MOJA YA MECHI ZAO ZA LIGI KUU TANZANIA BARA MSIMU HUU

Na Baraka Adson
Maafande wa Tanzania Prisons leo asubuhi wameshuka dimbani  katika uwanja wa TCC Sigara Chan`ombe kuvaana na Africa Lyon kwenye mechi ya kirafiki na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Bao pekee na la ushindi kwa Tanzania Prisons limefungwa na mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Elias Maguli kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza.


Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Katibu mkuu wa Tanzania Prisons, Sadick Jumbe alisema mchezo huo ulikuwa muhimu kwao kupima makali yao kabla ya kuwavaa Azam fc ambao wikiendi hii watakuwa nchini Liberia kuvaana wenyeji wao Barrack Controller II ya huko, mchezo wa kombe la shirikisho barani afrika.

"Kabla ya kucheza na Azam, tunahitaji mechi tano za kujipima uwezo, kesho tunacheza na Lyon lakini tunajiandaa pia kukutana na Ashanti United ili kujipima nao, huku tukitafuta mechi nyingine". Jumbe alisema.

Prisons wapo Ukonga jijini Dar es salaam kwenye maandalizi ya mchezo wao wa ligi kuu bara dhidi ya Azam fc ambao utachezwa machi 27 mwaka huu uwanja wa Chamazi Complex, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video