Wednesday, March 13, 2013

 ,
<<<<< AFRICAN LYON WAKUMBUSHIA MACHUNGU YA KUKATALIWA ZANTEL

KIKOSI CHA TANZANIA PRISONS

Na Baraka Adson

Maafande wa Tanzania Prisons kesho wanashuka dimbani mapema asubuhi katika uwanja wa TCC Sigara Chan`ombe kuvaana na Africa Lyon kwenye mechi ya kirafiki.

Prisons wapo Ukonga jijini Dar es salaam kwenye maandalizi ya mchezo wao wa ligi kuu bara dhidi ya Azam fc ambao utachezwa machi 27 mwaka huu uwanja wa Chamazi Complex, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Katibu mkuu wa Tanzania Prisons, Sadick Jumbe amesema mchezo huo ni muhimu kwao kupima makali yao kabla ya kuwavaa Azam fc ambao wikiendi hii watakuwa nchini Liberia kuvaana wenyeji wao Barrack Controller II ya huko, mchezo wa kombe la shirikisho barani afrika.

"Kabla ya kucheza na Azam, tunahitaji mechi tano za kujipima uwezo, kesho tunacheza na Lyon lakini tunajiandaa pia kukutana na Ashanti United ili kujipima nao, huku tukitafuta mechi nyingine". Jumbe alisema.

 Kwa upande wao Africa Lyon wamesema mchezo huo ni muhimu sana kwao hasa kwa wakati huu ambao wanahitaji kupata ushindi kwa mechi zilizosalia na kubakia ligi kuu Tanzania bara.

 
Katibu mkuu wa Africa Lyon, Ernest Brown alisema kwa mechi zilizosalia wana imani ya kufanya vizuri na wana mikakati ya kuijenga upya klabu hiyo.

Pia aliongeza kuwa tatizo kubwa lililosababisha timu ifanye vibaya msimu huu ni kutokana na mgogoro uliojitokeza baina ya aliyekuwa mdhamini wao mpya, kampuni ya simu za mkononi ya Zantel na Vodacom.

Zantel waliingia mkataba wa kuidhamini Lyon mwishoni mwa mwaka jana lakini mkataba wa Vodacom uliwabana kwa madai kuwa wao ni washindani wao hivyo hawaruhusiwi kuidhamini klabu hiyo.

Brown amesema kitendo hicho kiliwaathiri sana, kwani timu inashindwa kujiendesha kwa kukosa fedha, ikizingatiwa Vodacom wanatoa Milioni 7.5 kwa kila mwezi wakati timu inatumia milioni 26 kwa mwezi katika maandalizi na kuwalipa wachezaji posho.

Africa Lyon ni klabu iliyoanzishwa mwezi wa 6 mwaka 2000 kama Mbagara Market football club chini ya Jamal Kisongo, mwaka 2009 mwezi wa 11 ilimteua Charles Boniface Mkwasa kama kocha mkuu na iliwachukua wachezaji wengi kwa mkopo kutoka klabu tofauti kama Razack  Khalfan, Vincent Barnabas, Ulimboka Mwakingwe, Meshack Abel George Nyanda na Adam Kingwande.





0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video