Sunday, March 3, 2013


Na Baraka Adson
 
Ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2012/2013 inataraji kuendelea jumatano machi 6 kwa mechi tatu kupigwa.
Maafande wa JKT Oljoro wa mkoani Arusha watawakaribisha maafande wa Tanzania Prisons maarufu kama wajela jela kutoka jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sh. Amri Abeid Kaluta.
Kuelekea katika mchezo huo maafande wa Tanzania Prisons wakiwa na kumbukumbu ya kutoa suluhu pacha ya bila kufungana na wakata miwa wa manungu turiani mjini Morogoro, klabu ya soka ya Mtibwa sugar, wamesema kikosi chao kipo safi kuwakabili Oljoro ambao jana walipata matokeo ya suluhu dhidi ya Polisi Moro katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Katibu mkuu wa Tanzania Prisons, Sadick Jumbe amesema jana walikuwepo Jamhuri kuwaangalia wapinzani wao ili kuwasoma mchezo wao kabla ya kushuka nao dimbani wakiwa nyumbani kwao machi 6.
Ameongeza kuwa hakuna mchezaji mwenye kadi tatu na hakuna majeruhi hivyo kocha mkuu wa klabu hiyo Jumanne Chale atatumia wachezaji wote wa kikosi cha kwanza.
Pia Jumbe amesema tatizo lao la kupata sare nyingi ni suala la kawaida katika mchezo wa soka na hii inatokana na klabu nyingi sana kujiandaa vizuri hivyo kutoa changamoto nyingi sana.
Nao maafande wa Mgambo JKT wakiwa na machungu ya kufungwa mchezo uliopita 1-0 na Polisi Morogoro watakuwa nyumbani kuvaana na Mtibwa sugar ambao wana kumbukumbu ya kutoa suluhu wakiwa nyumbani kwao Manungu complex  dhidi ya maafande wa Tanzania prisons mchezo uliopita.
Antony Mgaya, katibu mkuu wa Mgambo JKT amesema timu yao ipo katika maandalizi makuba kuvaana na mtibwa sugar ambao ni wababe wa wazee wa Oman, klabu ya simba ya Dar es salaam katika msimu huu wa ligi lakini pia waliitikisa Yanga, wazee wa Uturuki.
Mgaya amesema mpaka sasa hakuna majeruhi na kocha mkuu wa klabu hiyo Mohamed Kampira anafanya marekebisho ya makosa yaliyojitokeza katika mchezo wao  dhidi ya Polisi Moro na kulala 1-0.
Pia amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza uwanja wa ccm Mkwakwani jijini Tanga ili kuishangilia timu yao.
Kwa upande wa Mtibwa sugar, kocha mkuu wa timu hiyo Merck Mexeme amesema kikosi chake kinajiandaa kufuta machungu ya kukosa mara nyingi matokeo ya ushindi na kuchukua alama 3 kwenye uwanja wa nyumbani.
Nahodha huyo wa zamani wa Mtibwa sugar na timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars amesema amefanya marekebisho ya kikosi chake na anajipanga kuwakung`uta Mgambo JKT wakiwa nyumbani kwao.
Mexeme amesema mpaka sasa hakuna majeruhi kwenye kikosi chake na anataraji kuwaduwaza Mgambo wakiwa kwao uwanja wa chama cha mapinduzi ccm Mkwakwani jijini Tanga.
Mchezo Mwingine wa ligi kuu machi 6 utakuwa katika dimba la Chamazi Komplex, jijini Dar es salaam baina ambapo African  Lyon watawakaribisha vijana wa kocha mzalendo Charles Boniface Mkwasa “Master” Maafande wa jeshi la kujenga taifa Ruvu shooting ambao katika mchezo uliopita walitoa suluhu na Wagosi wa kaya, Coastal Unioni katiba dimba la Mkwakwani.
Baada ya michezo ya jumatano machi 6, kesho yake machi 7 ligi itaendelea kwa mchezo mmoja, maafande wa Jkt Ruvu wataumana na Kagera Sugar vijana wa Abdlah King Kibaden “Mputa” mchezo utakaopigwa dimba la Azam Complex jijini Dar es salaam.
Jumatano Machi 6
JKT OLJORO v TANZANIA PRISONS [SH. AMRI ABEID, ARUSHA]
AFRICAN LYON FC v RUVU SHOOTINGS [AZAM COMPLEX, DAR ES SALAAM]
MGAMBO JKT v MTIBWA SUGAR [MKWAKWANI, TANGA]
Alhamisi Machi 7
JKT RUVU v KAGERA SUGAR [AZAM COMPLEX, DAR ES SALAAM]
Jumamosi Machi 9
YOUNG AFRICANS v TOTO AFRICANS [UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM]
AZAM FC v POLISI MOROGORO [AZAM COMPLEX, DAR ES SALAAM]
Jumapili Machi 10
SIMBA SC v COASTAL UNION [UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM]

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video