Saturday, March 2, 2013


>>BALE NDIO MTAMBO WA MAGOLI SPURS!!
>>VITA UBINGWA MANCHESTER: FERGIE AMDHIHAKI MANCINI!!
KESHO JIJI la London litazizima kwa Dabi ya Timu za London ya Kaskazini Uwanjani White Hart Lane wakati Tottenham na Arsenal zitakapocheza Mechi ya BPL, Barclays Premier League na huko Jijini Manchester, vita ya kisaikolojia kati ya Mahasimu Manchester City na Manchester United imezidi kupamba moto.
++++++++++++++++++++++
RATIBA
BPL: BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Jumamosi Machi 2
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v West Bromwich Albion
Everton v Reading
Manchester United v Norwich City
Southampton v Queens Park Rangers
Stoke City v West Ham United
Sunderland v Fulham
Swansea City v Newcastle United
[Saa 2 na Nusu Usiku]
Wigan Athletic v Liverpool
++++++++++++++++++++++
ARSENE WENGER ANAFURAHISHWA NA MASHAMBULIZI YAO
WENGER_AHIMIZA12Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameionya Tottenham ambayo wanapambana nayo kwenye Ligi Jumapili Uwanjani White Hart Lane kuwa Kikosi chake hakitegemei Mtu mmoja tu katika Mashambulizi yao.
Katika Misimu ya nyuma, Arsenal walikuwa wakimtegemea sana Robin van Persie kwa Magoli lakini sasa Wenger amedai Timu yake inao Wafungaji wengi tofauti na Tottenham mbayo sasa ni Gareth Bale ndio anaibeba Timu na ambae amefunga Bao 8 katika Mechi zake 6 za mwisho na Timu yake.
Mara ya mwisho Bale alifunga Bao la ushindi katika Dakika za mwisho Tottenham ilipoichapa West Ham Bao 3-2 Jumatatu iliyopita na kupanda na kuikamata nafasi ya 3 kwenye Ligi.
Pia, Wenger alithibitisha kutokuwa na mpango maalum wa kumdhibiti Bale na kusisitiza kuwa wao pia ni tishio katika ufungaji na wanasaka kutofungwa katika Mechi yao ya 6 mfululizo kwenye Ligi.
Wenger amesema: “Kwa sasa tuna uwezo wa kufunga kutoka Mchezaji yeyote na hilo ni safi kwangu. Tuna Wachezaji wengi wanaoweza kufunga. Walcott anaweza kufunga, Giroud anaweza kufunga, Cazorla anaweza kufunga, Podolski anaweza kufunga, na nadhani Wilshere pia!”
Aliongeza: “Tumefunga Goli nyingi zaidi kupita Msimu uliopita na Mwaka jana uwezo wetu  ulimtegemea Van Persie peke yake kufunga na Siku zote nilikuwa nikiogopa Siku ambayo Van Persie ataumia!”
SIR ALEX FERGUSON AMDHIHAKI ROBERTO MANCINI
Hivi majuzi, Meneja wa Manchester City, Roberto Mancini, alidai Man United wana bahati kuwaFERGIE_N_MANCINIPointi 12 mbele yao kileleni mwa Ligi lakini jana Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man United, alijibu mapigo na kumdhihaki mpinzani wake huyo.
Ferguson alitamka: “Ndio tuna bahati sana. Kwani tumekuwa tukifanya hivi kwa Miaka 25 tu! Ni tabia mbaya! Pengine Mancini ndie mwenye bahati kuwa Pointi 12 tu nyuma yetu!”
Jumamosi Man United wanaikwaa Norwich City Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi na ushindi kwao utawafikisha Pointi 15 mbele ya Man City ambao wanacheza Mechi yao ya Ligi Jumatatu Usiku ugenini na Aston Villa.
++++++++++++++++++++++
RATIBA
BPL: BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Jumapili Machi 3
[Saa 1 Usiku]
Tottenham Hotspur v Arsenal
Jumatatu Machi 4
[Saa 5 Usiku]
Aston Villa v Manchester City
++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 27]
1 Man United Pointi 68
2 Man City 56
3 Tottenham 51
4 Chelsea 49
5 Arsenal 47
6 Everton 42
7 WBA 40
9 Liverpool 39
9 Swansea 37
10 Stoke 33
11 Fulham 32
12 Norwich 32
13 Newcastle 30
14 West Ham 30
15 Sunderland 29
16 Southampton 27
17 Wigan 24
+++++++++++++++++++
18 Aston Villa 24
19 Reading 23
20 QPR 17
++++++++++++++++++++++

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video