Wednesday, March 6, 2013

>>ILISTAHILI AU LA??
FERGIE_n_MOURINHOManchester United wamebwagwa nje ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa Jumla ya Bao 3-2 katika Mechi mbili na Real Madrid baada ya jana kufungwa Bao 2-1 Nyumbani kwao Old Trafford katika Mechi waliyokuwa wakiongoza 1-0 na Winga wao Nani kutwangwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 56 na hapo ndipo Gemu ikaangukia kwa Real waliotandika Bao mbili za haraka katika Dakika za 66 na 69.
Real Madrid sasa wanasonga mbele kuingia Robo Fainali na kuacha mjadala mkubwa kuhusu uhalali na kama ni haki kwa Refa toka Uturuki, Cuneyt Cakir, kutoa Kadi Nyekundu kwa Nani na kuwavuruga Man United na kuirahisishia Real kupata ushindi.
TUKIO LENYEWE
Katika Dakika ya 56, Nani aliruka juu huku macho yake yakiangalia Mpira na ilionekana hakumwona Alvaro Arbeloa na Mguu wake kumgonga Beki huyo wa Real.
Bila kutarajiwa Refa Cuneyt Cakir akampa Nani Kadi Nyekundu na kuwaacha Man United wakiwa Mtu 10.
REFA
Kwa Cuneyt Cakir, hii ilkuwa Mechi yake ya tatu kuichezesha Manchester United nyingine zikiwa Msimu uliopita dhidi ya Athletic Bilbao kwenye EUROPA LEAGUE na Benfica kwenye UCL.
Mechi hizo hazikuwa na matukio makubwa.
Mwaka jana, kwenye Mechi ya Pili ya Nusu Fainali ya UCL, Cakir alimtoa nje kwa Kadi Nyekundu Nahodha wa Chelsea John Terry awalipocheza na Barcelona huko Camp Nou, na pia kumlima Kadi Nyekundu Mario Balotelli wakati Manchester City inawafunga Bao 1-0 Dinamo Kiev Mwaka 2011.
Cakir pia alichezesha Nusu Fainali ya EURO 2012 kati ya Portugal na Spain na awali kwenye hatua ya Makundi ya Mashindano hayo alishawahi kumpa Kadi Nyekundu Keith Andrews wa Republic of Ireland walipocheza na Italy.
NINI WAMESEMA
-Jose Mourinho, Kocha wa Real Madrid: “Sizungumzii tukio hilo. Timu Bora imepoteza. Hii ndio Soka!”
-Roy Keane, Nahodha wa zamani wa Man United: "Refa alifanya uamuzi sahihi. Kila Mtu ameudhiwa, ni bahati mbaya lakini ni Mchezo hatari Ni Kadi Nyekundu. Hata kama humuangalii adui yako, kumgonga vile ni kosa!”
-Dermot Gallagher, Refa Mstaafu: "Uamuzi ule ulikuwa mkali mno. Na yule Mchezaji wa Real alikandamiza uamuzi ule kwa jinsi alivojifanya baada ya kugongana. Nani hakumgusa kifuani, ni mkononi kama alivyojifanya Arbeloa baada ya kuanguka. Hamna haja kusisitiza Nani alikuwa akiangalia mpira tu, hakukusudia kucheza rafu. Kama ni kutoa Kadi basi ni Kadi ya Njano! Ningekuwa mimi nachezesha nisingemtoa!”
-Mike Phelan, Msaidizi wa Sir Alex Ferguson: “Meneja hayupo hapa na hayupo kwenye hali ya kuongelea uamuzi wa Refa. Hilo linaonyesha waziwazi nini anafikiria kuhusu uamuzi ule. Ni uamuzi mkali, ni wa kushangaza kwa wakati ule wa Mechi!”
-David Moyes, Meneja wa Everton: “Nadhani leo Sir Alex Ferguson atakuwa amekasirika kupita kiasi. Wachezaji wa Man United walikuwa na haki kumzonga Refa kwa uamuzi ule. Ulikuwa uamuzi mbovu uliowafanya wapoteze Mechi kubwa. Hata Wachezaji wa Real hawakutegemea Kadi Nyekundu!”
kutoka soka in Bongo

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video