Sunday, March 10, 2013

picha na Bin Zubeiry

Didier Kavumbangu wa Yanga, akiruka kwanja la  beki wa Toto, Everist Maganga katika mechi ya jana.

Na Boniface Wambura
MVUA iliyonyesha jana kutwa nzima, imeathiri kwa kiasi kikubwa mapato ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana kati ya wenyeji Yanga na Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ni watazamaji 7,412 tu waliojitokeza jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kushuhudia mechi hiyo ya timu ndugu na kufanya mapato ya jumla yaliyopatikana yawe ni Sh. 42,508,000 tu.
Mechi hiyo namba 135 iliyochezeshwa na Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani ilimalizika kwa Yanga ambao wanaongoza VPL wakiwa na pointi 45 kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 9,406,764.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 6,484,271.19.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 6,708 na kuingiza sh. 33,540,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 89 na kuingiza sh. 1,780,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 4,783,100.82, tiketi sh. 4,136,390, gharama za mechi sh. 2,869,860.49, Kamati ya Ligi sh. 2,869,860.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,434,930.25 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,116,056.86.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video