KLABU ya Arsenal imeongeza matumaini ya kucheza Ligi ya mabingwa kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Emirates, ambao unawapeleka The Royals mkiani mwa Ligi Kuu England.
Katika mchezo huo, mabao ya Arsenal yalifungwa na Gervinho dakika ya 11, Cazorla dakika ya 48, Giroud dakika ya 67 na Arteta dakika ya 77, wakati bao pekee la kufutia machozi la Reading lilifungwa na Robson-Kanu dakika ya 68.
Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa; Fabianski, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Monreal/Gibbs dk71, Arteta, Rosicky, Ramsey, Gervinho/Oxlade-Chamberlain dk75, Cazorla na Giroud/Podolski dk75.
Reading: Taylor, Kelly, Pearce, Mariappa, Shorey, Leigertwood, Karacan/Akpan dk76), Guthrie, McAnuff, Robson-Kanu/McCleary dk80) na Pogrebnyak/Hunt dk61.
Pointi tatu: Bacary Sagna akimpongeza Gervinho baada ya kuifungia Arsenal bao la kwanza
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Chelsea ililala 2-1 mbele ya Southampton kwenye Uwanja wa St Mary's, mabao ya washindi yakitiwa kimiani na Rodriguez dakika ya 23 na Lambert dakika ya 35, wakati la kufutia machozi la The Blues likifungwa na John Terry dakika ya 33.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa;Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Terry, Bertrand, Mikel/Ramires dk71, Lampard, Moses, Oscar/Benayoun dk76, Marin/Hazard dk60 na Torres.
Southampton: Boruc/Kelvin Davis dk46, Clyne, Yoshida, Hooiveld, Shaw, Puncheon/Ward-Prowse dk62, Schneiderlin, Cork, Steven Davis/Fox dk85, Rodriguez na Lambert.
Pigo: Wachezaji wa Chelsea wakiwa hoi baada ya kipigo
Tottenham Hotspur imeshinda 2-1 dhidi ya Swansea, mabao yake yakitiwa kimiani na Vertonghen dakika ya saba na Bale dakika ya 21, wakati la wapinzani wao lilifungwa na Michu dakika ya 71.
Gareth Bale (kulia) akiifungia Tottenham bao la pili
West Ham United imeshinda 3-1 dhidi ya West Bromeich, mabao yake yakitiwa kimiani na Carroll dakika ya 16 na 80 na O'Neil dakika ya 28, wakati la kufutia machozi la wapinzani wao lilifungwa na Dorrans dakika ya 88 kwa penalti.
Shangwe za ushindi: Wachezaji wa West Ham wakimpongeza Carrol baada ya kufunga bao la pili
Manchester City imeshinda 4-0 dhidi ya Newcastle, mabao yake yakifungwa na Carlos Tevez dakika ya 41, David Silva dakika ya 45, Nahodha wake, Vincent Kompany dakika ya 56 na Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure dakika ya 59.
Asante Kompany: Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany akipongezwa na wenzake kwa kufunga
0 comments:
Post a Comment