Thursday, March 14, 2013


Kushoto juu ni Malkia wa Nyuki, kulia kikosi kinachotumika kwa sasa Simba SC na chini ni 'Mafaza' waliotengwa; kutoka kulia Redondo, Nyosso, Kazimoto, Maftah na Boban.

Kutoka kwa Bin Zubeiry

MWENYEKITI wa Kamati Maalum ya kuhakikisha Simba SC inafanya vyema katika wakati huu mgumu, Rahma Al Kharoos ‘Malkia wa Nyuki’ ameanzisha mpango wa ‘Tajirika na Ushindi’ kwa wachezaji wa timu hiyo.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Malkia huyo alisema kwamba amekuja na mpango wa Tajirika na Ushindi, ambao wachezaji wakishinda wanapata donge nono.
“Mpango huu umeanza tangu mechi na Coastal Union, niliwachafua wachezaji kwa mamilioni ya fedha baada ya kushinda. Na utaendelea hadi mwisho wa Ligi Kuu,”alisema Malkia.
Mama huyo alisema kwamba kwa sasa anaelekeza nguvu zake katika mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba mkoani Kagera Machi 27, mwaka huu.
Amesema anafurahia maendeleo ya timu ambayo kwa sasa inaundwa na vijana wengi waliopandishwa kutoka kikosi cha pili na anaamini itafanya vizuri.
“Wale vijana walicheza soka ya kiwango kikubwa sana mechi na Coastal, kila mtu alijionea na ile mechi ilikuwa ngumu sana, lakini walishinda,”alisema.
Simba SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, wako hatarini kupoteza taji lao hilo kutokana na kuachwa mbali na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.
Yanga SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 45, wakati Simba SC ina pointi 34 timu zote zikiwa zimecheza mechi 20 wakati Azam FC yenye pointi 37, inashika nafasi ya pili.
Simba SC ambayo inaelekea kukata tamaa ya ubingwa, lakini inaonekana kutaka kupigana japo ikamate nafasi ya pili, ili iweze kucheza Kombe la Shirikisho mwakani. 
Hata hivyo, kocha Mfaransa, Patrick Liewig amewasimamisha baadhi ya wachezaji wakubwa wa timu hiyo, wakiwemo mabeki Amir Maftah, Juma Nyosso, viungo Haruna Moshi ‘Boban’, Mwinyi Kazimoto na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kutokana na nidhamu yao mbovu.
Kikosi cha Simba hivi sasa kinaundwa zaidi na nyota waliopandishwa kutoka timu ya vijana, maarufu kama Simba B, ambao ndio waliipiga Coastal Union 2-1 na kunufaika na mamilioni ya Malkia wa Nyuki.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video