SIMBA |
Na Baraka Mpenja
Jahazi la mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara,
wekundu wa Msimba Simba SC “Taifa Kubwa” lazidi kutota baada ya leo hii kulazimisha
sare ya mabao 2-2 na watoto wa mitaa ya kishamapanda Toto Africa, katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara
uliopigwa ndani ya dimba CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Mabao ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na kinda wake
Rashidi Mkoko, dakika ya 28 kipindi cha kwanza na bao la pili likafungwa dakika ya 62 kupitia kwa winga wake machachari na
mwenye mbio nyingi “Anko” Mrisho Khalfan Ngasa.
Mabao ya Toto yalifungwa na
Mrisho Musa dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza na mwokozi wa Toto leo hii
ni Seleman Kibuta aliyetia kambani bao maridhawa la kuzawzisha dakika ya 74 ya
kipindi cha pili na kurudisha machungu kwa mashabiki wa Simba waliojimwaga kwa
wingi leo hii kirumba.
Matokeo mengine, katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro,
wazee wa Uturuki na vinara ya ligi kuu soka Tanzania bara wamefikisha pointi 49
kileleni baada ya kushindwa kuwapigisha kwata maafande wa Polisi Morogoro kwa
kulazimisha suluhu ya bila kufungana.
YANGA |
Mabatini Mlandizi mkoani Pwania maafande wa Charles Boniface
Mkwasa “ Master” wamelambishwa koni za Azam baada ya kukubali bakora 1-0 kutoka
kwa lambalamba ambao bao lao lilifungwa dakika ya 44 kipindi cha kwanza kupitia
kwa Kipre Tchetche na kufikisha pointi 43 katika nafasi ya pili.
Katika dimba la Kaitaba,wana “Ngulukumbi” wa Kagera sugar
wakinolewa na winga machachari wa zamani wa klabu ya Simba miaka ya sabini na
timu ya taifa ya Tanzania , Taifa stars, Abdallah Kibadeni “king Mputa”
wametafuna miwa ya ndugu zao wa Mashamba ya miwa ya Manungu, Mtibwa sugar, baada
ya kuwatandika mabao 3-0 wakiwa nyumbani kwao.
Mbao ya Kagera yametiwa kambani na Maregesi Mwangwa dakika
ya 1 ya mchezo na Themi Felix katika
dakika ya 35 na 67. Bao la kupunguzia machungu kwa Mtibwa sugar limefungwa
na Vicent Barnabas katika dakika ya 50
ya mchezo huo.
Hata hivyo Meneja wa Mtibwa sugar, David Bugoya amelalamikia
kitendo cha mwamuzi wa mchezo hu kuwaonesha wachezaji wake wawili kadi nyekundu
kipindi cha pili na kuwazawadia mkwaju wa penati kagera sugar.
Bugoya alisema
wameonewa katika mchezo huo na kama waamuzi wataendelea kufanya madudu hayo,
wataliweka rehani soka letu ambalo linahitaji mabadiliko makubwa.
MTIBWA SUGAR |
Matokeo mengine, Katika dimba la Sh. Amri Kuluta Abeid mjini Arusha, maafande wa JKT Oljoro
wamewapigisha kwata maafande wenzao wa JKT Ruvu baada ya kuwadungua 2-0
nyumbani.
Mabao ya Oljoro yamezamishwa na Idd Swalehe dakika ya 4 ya
mchezo, na la pili likatupiwa nyavuni na Paul Nongwa.
Hapa Dar es salaam katika dimba la Azam Chamazi, African Lyon wamepata ushindi
wa pili mfululizo baada ya kuwabamiza wagosi wa kaya Coastal union ya Tanga bao
1-0 likifungwa na nyota wake Adam Kingwande.
AFRICAN LYON |
WAGOSI WA KAYA |
0 comments:
Post a Comment