^^^6KUIVAA
BARRACK YOUNG CONTROLLERS II MACHI 15, 16 AU 17!!
Makocha Keny Mwaisabula "mzazi" na John Wiliam "DEl Piero" anayenikonoa kikosi cha mabingwa wa zamani wa Tanzania African Sports ya Tanga na mjumbe wa kamati ya ufundi ya Simba kwa nyakati tofauti wameipongeza klabu ya soka ya Azam fc kufuzu raundi ya pili ya kombe la shirikisho barani afrika.
Piero kwa upande wake ameiambia MATUKIO DUNIANI kuwa Azam fc wanatakiwa kuuchukulia ushindi wa 3-1 wakiwa nyumbani na 5-0 swakiwa sudan ya kusini dhidi ya wapinzani wao Al Nasri Juba kombe la shiriksho kama changamoto kwao kujipanga zaidi.
"siku zote unaweza kuanza na timu ngumu raundi ya kwanza na raundi inayofauata ukapangwa na timu ngumu zaidi, hivyo Azam wasibweteke licha ya kuwa na kikosi bora kwa sasa, kinachotakiwa ni kujiandaa kwa nguvu zote." Piero alishauri.
Pia kocha huyo aliongeza kuwa Azam wanatakiwa kukaribisha ushauri wa kiufundi kutoka kwa makocha na wadau wa soka ili kuendelea kuwakilisha kwa uzuri jamhuri ya muungano wa Tanzania medani ya soka barani afrika.
Mwaisabula kwa upande wake alisema Azam fc imetoa fundisho kwa mashabiki na viongozi wa soka kuwa soka halipo huku wanakodhani zaidi.
Aliongeza kuwa viongozi wake wamejipanga vizuri na ndio maana walitanguliza mapema viongozi wao sudan ya kusini ili kujua mazingira ya kule watachezea wapi, watakula nini na watalala wapi kitu ambacho ni gharama kubwa sana.
"Azam inastahilki pongezi kwa kitendo hicho cha kimapinduzi, binafs nimefarijika sana kwa ushindi wao, nawatakia kila la heri katika michuano hiyo". Mwaisabula alitia baraka zake.
Wakati huo huo nalo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) linatoa pongezi kwa timu ya Azam ya Tanzania Bara kwa kufanikiwa
kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho iliyo chini ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Ushindi wa jumla ya mabao 8-1 ambao Azam
imeupata dhidi ya Al Nasir Juba ya Sudan Kusini si fahari kwa timu hiyo
tu, bali Tanzania kwa ujumla, na unaonyesha jinsi klabu hiyo
ilivyojipanga kiushindani katika michuano hiyo ya Afrika.
Hata hivyo, ni vizuri Bodi ya
Wakurugenzi ya klabu hiyo, benchi la ufundi na wachezaji wa timu hiyo
wakautazama ushindi huo kama changamoto kwao kuhakikisha wanajipanga
vizuri zaidi kwa raundi inayofuata.
Timu ya Azam inayofundishwa na
Mwingereza John Stewart Hall ilishinda nyumbani mechi ya kwanza mabao
3-1, na jana kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 ugenini jijini Juba.
Kwa kufanikiwa kuing’oa Al Nasir Juba,
Azam sasa watacheza raundi ya kwanza (raundi ya 16 bora) ya michuano
dhidi ya Barrack Y.C.II ya Liberia ambayo katika raundi ya awali iliitoa
Johansens ya Sierra Leone. Barrack ilishinda bao 1-0 nyumbani katika
mechi ya kwanza na kulazimisha suluhu katika mechi ya marudiano jijini
Freetown.
Azam itaanzia mechi hiyo ugenini kati ya
Machi 15,16 na 17 mwaka huu wakati mechi ya marudiano itachezwa
Tanzania kati ya Aprili 5,6 na 7 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment