MOJA YA KIKOSI CHA TAIFA STAR KATIKA MECHI ZILIZOPITA |
Kiingilio
cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania
(Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Jumapili
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya
kijani.
Viti
vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000
viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni
sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897
ni sh. 10,000.
Viingilio
vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni
sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A
yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000.
Tiketi
kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza
kuuzwa siku mbili ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo
vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa
wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta
Buguruni na Dar Live Mbagala.
Katika
vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia
yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi. Vilevile tunapenda
kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika
maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa
fursa ya kushuhudia mechi hiyo.
KIKOSI CHA MORROCO |
SAMATA, ULIMWENGU WARIPOTI STARS
MBWANA SAMATA |
Washambuliaji
wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya
TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili nchini
jana usiku na kwenda moja kwa moja kambini.
Ujio
wa washambuliaji hao unafanya idadi ya wachezaji walioripoti kambini
kufikia 20 kati ya 23 walioitwaa baada ya mshambuliaji Khamis Mcha
aliyekuwa na kikosi cha timu yake ya Azam nchini Liberia naye kuripoti
kambini leo asubuhi.
Wachezaji
John Bocco na makipa Mwadini Ally na Aishi Manula ambao pia nao
walikuwa Liberia na timu yao ya Azam wataripoti kambini leo alasiri.
Wachezaji hao ni sehemu ya msafara wa timu ya Azam ambao utakuja na
ndege ya mchana kutokea Nairobi kwa vile ile ya asubuhi waliyotangulia
nayo wenzao kuwa imejaa.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha
Kim Poulsen leo inaendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa. Mazoezi hayo
yataanza saa 9 alasiri.
KOCHA WA STARS, KIM PAULSEN AKIWA NA SAMATA KATIKA MOJA YA MAZOEZI YA TIMU YAKE |
TIMU TATU ZASHUKA DARAJA FDL
Timu
tatu zimeshuka daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kurudi Ligi ya
Mkoa msimu ujao wa 2013/2014 baada ya kushika nafasi za mwisho katika
ligi hiyo msimu huu 2012/2013 iliyomalizika wikiendi iliyopita.
Small
Kids ya Rukwa imeporomoka kutoka kundi A baada ya kuondolewa kwenye
michuano hiyo mapema kwa kushindwa kufika uwanjani kwenye moja ya mechi
zake. Kwa mujibu wa kanuni matokeo yote ya mechi ilizocheza yalifutwa.
Moro
United ya Dar es Salaam ndiyo iliyoaga FDL kutoka kundi B baada ya
kumaliza mechi zake ikiwa na pointi tatu. Wakati kutoka kundi C timu
iliyoshuka ni Morani ya Manyara iliyomaliza ligi ikiwa na pointi kumi na
moja.
Timu
zilizopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2013/2014 ni
Mbeya City ya Mbeya iliyoongoza kundi A ikiwa na pointi 31, vinara wa
kundi B timu ya Ashanti United ya Dar es Salaam yenye pointi 29 wakati
Rhino Rangers ya Tabora imepanda kutoka kundi C ikiwa na pointi 32.
LIUNDA KUTATHIMINI WAAMUZI KOMBE LA DUNIA
Mwamuzi
Msaidizi wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Leslie Liunda ameteuliwa
kuwa mtathimini wa waamuzi (referee assessor) kwenye moja ya mechi za
mchujo za Kombe la Dunia.
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Liunda kutathimini
waamuzi kwenye mechi kati ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na
Libya itakayochezwa Jumapili (Machi 24 mwaka huu).
Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Martyrs jijini Kinshasa kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika ya Kati (CAT).
Waamuzi
watakaochezea mechi hiyo William Selorm Agbovi atakayekuwa mwamuzi wa
kati, Malik Alidu Salifu (mwamuzi msaidizi namba moja), David Laryea
(mwamuzi msaidizi namba mbili) na mwamuzi wa mezani (fourth official)
Cecil Amatey Fleischer. Waamuzi wote hao wanatoka Ghana.
0 comments:
Post a Comment