By Baraka Mpenja
Ni vita ya kufa na kupona kati ya
watengeneza sukari nchini Tanzania klabu ya Mtibwa Sugar dhidi ya Kagera Sugar
watakaokuwa na kazi ngumu ya kuwania pointi tatu muhimu katika mchezo wa ligi
kuu soka Tanzania bara.
Pambano hilo la watengeneza sukari
sukari limevuta hisia za mashabiki lukuki wa soka kwa mikoa ya kanda ya ziwa Victoria
huku likitarajiwa sehemu ya kufurahia
katika mapumziko ya pasaka.
KAGERA SUGAR |
Akizungumza kutoka mkoani Kagera,
kocha mkuu wa Mtibwa sugar na nahodha wa zamani wa timu hiyo pamoja na timu ya
taifa ya Tanzania (Taifa Stars), mzalendo Merck Mexeme amesema maandalizi ya
mchezo huyo yamefanyika kwao Manungu na leo hii wanapasha moto misuli baada ya
safari ndefu ya siku mbili kuelekea mkoani humo.
Mexme alisema soka siku zote ni
maandalizi, wao wamejipanga vizuri na bahati nzuri hakuna mchezaji ambaye yuko
hatarini kuukosa mchezo huo unaotabiriwa kuwa mgumu sana.
“Kagera ni timu nzuri na wana kocha
mzuri, mzee Abdallah King Kibadeni ambaye alinifundisha hata mimi, ana mbinu
nyingi sana lakini kwa kuwa aliwahi kuwa mwalimu wangu, nitatumia mbinu zake
kumfunga akiwa nyumbani kwake hapo kesho”. Alisema kocha Mexeme .
Mexeme ambaye ni kocha aliyejijengea
heshima kubwa akiwa mchezaji na sasa kocha wa Mtibwa sugar aliongeza kuwa kesho
atapanga kikosi chake cha matumaini na anawapanga vijana wake kupambana na
Kagera Sugar ambao watakuwa mbele ya umati mkubwa wa mashabiki ambao ndio siri
ya matokeo unapocheza uwanja wa nyumbani.
Naye mshambuliaji mahiri wa tanzania
miaka ya nyuma huku akivuma na kupewa jina la king Mputa akiwa na klabu ya Simba
akicheza kama winga mahiri miaka ya sabini na sasa ni kocha wa watengeneza miwa
pacha wa mtibwa, Kagera Sugar “ wanangulukumbi” Abdallah Kibaden akiongea kwa kujiamini baada
ya kutoa dozi kwa simba SC amesema kuwa mchezo wao wa kesho wanataraji kuwapa
zawadi ya pasaka mashabiki wao.
“Mara baada ya kuifunga simba goli 1-0, vijana
wangu wana kila sababu ya kuongeza wigo wa tofauti ya pointi kati yetu na
Mtibwa ,Wanahitaji sana ushindi katika
mchezo wa kesho, malengo yetu ni kupata nafasi mojawapo ya kuwakilisha nchi medani ya kimataifa”. Alisema king Mputa.
Nao mabingwa watetezi wa taji wekundu
wa Msimbazi Simba “Taifa Kubwa” baada ya kipigo cha 1-0 sasa watakuwa na kazi
pevu katika nyasi nzuri za uwanja wa CCM Kirumba kudadavuana na watoto wa mitaa
ya Kishamapanda Toto Africa.
MTIBWA SUGAR |
Simba watashuka
Kirumba wakitaka kuonesha uwezo wao na manjonjo ya vijana wake mbele ya mapacha
hao wa vinara wa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es
Salaam.
Tayari timu tatu za Mbeya city ya
jijini Mbeya, Ashant United ya Dar es Salaam na Rhino Rangers ya Tabora zimeshakata tiketi
ya kucheza mitanange ya ligi kuu msimu
ujao, huku timu tatu za ligi zikisubiri kupitiwa na fagio la chuma.
Timu za African Lyon, Polisi Morogoro,
JKT Ruvu, Tanzania Prisons, Mgambo shooting na JKT Oljoro zinaonekana kuchuana
vikali kukwepa mkasi wa kurejea ligi daraja la kwanza Tanzania bara (FDL).
0 comments:
Post a Comment