Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaipongeza klabu ya Azam kwa ushindi wa
mabao 2-1 ilioupata timu yake katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya
Kombe la Shirikisho.
Mechi
hiyo dhidi ya Barrack Young Controllers II ilichezwa jana jijini Monrovia, na
timu hizo zitarudiana wikiendi ya Aprili 6 au 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Ushindi
huo unaiweka Azam chini ya kocha wake Stewart John Hall katika mazingira mazuri
ya kusonga mbele baada ya mechi ya marudiano. Bila shaka ushindi wa timu ya
Azam pamoja na mambo mengine umechangiwa na klabu hiyo kujipanga vizuri.
Hata
hivyo ushindi huo bado ni changamoto kwa wachezaji, benchi la ufundi na uongozi
wa Azam kuhakikisha unajipanga vizuri kwa mechi ya marudiano kwa vile mpira wa
miguu una matokeo ya aina tatu; kushinda, kutoka sare au kufungwa.
Msafara
wa timu ya Azam unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Blassy
Kiondo unatarajiwa kurejea nchini kesho alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways
kupitia Nairobi.
TAIFA
STARS TRAINING PROGRAMME
Taifa
Stars itacheza mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la
Dunia mwaka nchini Brazil dhidi ya Morocco. Mechi hiyo itachezwa Jumapili
katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Jumamosi,
Machi 16- Wachezaji kuanza kuripoti kambini
Jumapili,
Machi 17- Mazoezi Uwanja wa Karume- Saa 2 asubuhi
Jumatatu,
Machi 18- Mazoezi Uwanja wa Karume- Saa 9 alasiri
Jumanne,
Machi 19- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Jumatano,
Machi 20- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 2 asub na saa 9 alasiri
Alhamisi,
Machi 21- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Ijumaa,
Machi 22- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Jumamosi,
Machi 23- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 10.30 jioni
PONGEZI
KWA UONGOZI MPYA TAFCA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha
Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) uliochaguliwa katika uchaguzi
uliofanyika juzi (Machi 16 mwaka huu) mjini Dodoma.
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa TAFCA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia taaluma
ya ukocha nchini.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TAFCA chini ya
uenyekiti wa Oscar Don Koroso aliyeibuka mshindi kwa kura zote za ndiyo baada
ya kukosa mpinzani.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli
za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba ya TAFCA pamoja na vyombo vya mpira wa
miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA chini ya Ramadhan Mambosasa na
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu
wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu
nzima ya uongozi wa TAFCA iliyochaguliwa inaundwa na Dk. Oscar Dan Koroso
(Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala (Katibu
Mkuu), Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Dismas Haonga (Mhazini), Wilfred Kidao
(mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF).
Wajumbe
wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa ni Jemedari Saidi, George Komba na Magoma
Rugora.
0 comments:
Post a Comment