>>HODGSON KUONGEA NA MAN UNITED KUHUSU RIO!
BOSI wa England Roy Hodgson amesisitiza kuwa sare ya 1-1 waliyopata huko Podgorica na Montenegro
na kuwaacha nafasi ya Pili, Pointi 2 nyuma ya Montenegro, bado haijaua
matumaini yao ya kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka
2014.
+++++++++++++++++++++
KUNDI H
[Kila Timu Mechi 6 isipokuwa inapotajwa]
1 Montenegro Pointi 14
2 England 12
3 Poland Mechi 5 Pointi 8
4 Ukraine Mechi 5 Pointi 8
5 Moldova 4
6 San Marino 0
+++++++++++++++++++++
Hodgson ametamka: “Bado ipo mikononi
mwetu-bado kucheza na Montenegro Wembley, Poland Nyumbani na Ukraine
ugenini. Tuna Gemu 3 Nyumbani na tutajaribu kushinda hizo.”
Kwenye Mechi hiyo huko Podgorica,
England walianza vyema kwa kufunga Bao mapema kupitia Wayne Rooney
katika Dakika ya 6 na kutawala Kipindi cha Kwanza na kukosa nafasi
kadhaa kuongeza Mabao.
Kipindi cha Pili, Montenegro walibadilika hasa baada ya kuingizwa Dejan Damjanovic ambae ndie alisawazisha katika Dakika ya 78.
+++++++++++++++++++++
MECHI ZA ENGLAND ZILIZOBAKI KUNDI H:
Septemba 6: England v Moldova
Septemba 10: Ukraine v England
Oktoba 11: England v Montenegro
Oktoba 15: England v Poland
+++++++++++++++++++++
Hii ni mara ya pili kwa England kuumwaga
uongozi huko Podgorica kwani Oktoba 2011, waliongoza Bao 2-0 dhidi ya
Montenegro, wakiwa chini ya Kocha Fabio Capello, na kuiruhusu Montenegro
kusawazisha na Mechi kwisha 2-2 lakini sare hiyo, na Pointi hiyo moja,
iliwaingiza Fainali za EURO 2012.
RIO FERDINAND
WAKATI HUO HUO, Roy Hodgson, alipoulizwa
kuhusu hatima ya Beki wa Manchester United Rio Ferdinand kuichezea
England, hasa baada ya safari hii kuitwa na kujitoa akitaja sababu za
kiafya, alijibu kuwa ataongea na Klabu ya Manchester United kuhusu
uimara wa Beki huyo.
Hodgson amesema: “Ikiwa atacheza baadae inabidi tuzungumze na Klabu yake.”
Kwenye Mechi na Montenegro, Masentahafu
walikuwa Joleon Lescott wa Man City na Chris Smalling wa Man United na
Hodgson alisisitiza walicheza vizuri mno.
0 comments:
Post a Comment