>>ROVERS v MILLWALL KURUDIANA JUMATANO EWOOD PARK!
>>CHELSEA v MAN UNITED, STAMFORD BRIDGE, TAREHE KUPANGWA!!
MARA
baada ya Mechi mbili za Robo Fainali ya FA CUP, ambazo zote leo
zimetoka sare kwa Manchester United kutoka 2-2 na Chelsea na Milllwall
na Blackburn Rovers kumaliza 0-0, Droo ya Nusu Fainali imefanyika na
Mshindi kati ya Chelsea na Man United atacheza na Man City na nyingine
Mshindi kati ya Blackburn Rovers na Millwall atavaana na Wigan.
Katika RobO fainali mbili zilizochezwa jana Wigan iliifunga Everton Bao 3-0 na Man City kuirarua Barnsley Bao 5-0.
Nusu Fainali zote mbili zitachezwa Uwanja wa Wembley JijinI london hapo Aprili 13 na 14.
MAN UNITED 2 CHELSEA 2
WAKIWA kwao Old Trafford, Manchester
United waliongoza kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Chicharito na Wayne Rooney
lakini Chelsea walichachamaa na kusawazisha Bao zote kupitia Eden Hazrd
na Ramires.
Mechi hii sasa itarudiwa Uwanjani Stamford Bridge katika Tarehe itakayopangwa.
VIKOSI:
MAN UNITED: De Gea; Rafael, Evans, Ferdinand, Evra; Nani, Carrick, Cleverley, Kagawa; Rooney, Hernandez
Akiba: Amos, Valencia, Anderson, Vidic, Young, Welbeck, van Persie.
CHELSEA: Cech; Azpilicueta, Luiz, Cahill, Cole; Ramires, Lampard; Moses, Mata, Oscar; Ba
Akiba: Turnbull, Ivanovic, Torres, Mikel, Hazard, Terry, Bertrand.
Refa: Howard Webb
MILLWALL 0 BLACKBURN 0
Millwall na Blackburn Rovers itabidi
zirudiane Jumatano hii Uwanjani Ewood Park, Nyumbani kwa Rovers, baada
ya kutoka sare 0-0 Uwanjani kwa Millwall kwenye Robo Fainali ya FA CUP.
Millwal ndio walitawala Mechi hii na Andy Keogh kupita posti lakini hakuna Timu iliyopata Bao hadi Dakika 90 zinamalizika.
VIKOSI:
Millwall: Forde, Dunne,
Shittu, Beevers, Lowry, Jack Smith, Trotter, Chris Taylor, N'Guessan,
Hulse, Keogh. Subs: Maik Taylor, Marquis, Feeney, Adam Smith, Abdou,
Osborne, Saville.
Blackburn: Kean,
Henley, Dann, Grant Hanley, Markus Olsson, Bentley, Lowe, King,
Pedersen, Rhodes, Best. Subs: Sandomierski, Orr, Givet, Dunn, Nuno
Gomes, Rekik, Goodwillie.
Refa: Martin Atkinson
0 comments:
Post a Comment