Saturday, March 2, 2013

>>UWANJA: EL ESTADIO SANTIAGO BERNABEU, SAA 12 JIONI
>>XAVI NJE, MESSI KUCHEZA LICHA YA HOMA!!
>>MOURINHO KUPANGUA KIKOSI, KUIVIZIA MAN UNITED!!
MESSI_n_RONALDO-2MACHI13NDANI YA Siku 4 baada ya Real Madrid kuichapa Barcelona Bao 3-1 Uwanjani Nou Camp na kuwatupa nje ya COPA del Rey, leo tena Timu hizo zinakumbana safari hii ndani ya Uwanja wa Santiago Bernabeu kwenye Mechi ya La Liga.
Real Madrid, ambao ndio Mabingwa watetezi wa La liga, wako nafasi ya 3 kwenye Ligi hiyo inayoongozwa na Barcelona ambao wako Pointi 16 mbele ya Real na Pointi 12 mbele ya Timu ya Pili Atletico Madrid.
ZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU KUHUSU MECHI HII:
HALI ZA WACHEZAJI:
Real Madrid inaweza ikawachezesha Marcelo, Luka Modric, Kaka na Karim Benzema ambao wote hawakucheza waliposhinda 3-1 kwenye Copa del Rey Jumanne huko Camp Nou.
Pia Beki Sergio Ramos, baada ya kutumikia Kifungo cha Mechi 1, anaweza kucheza lakini Winga Angel Di Maria hatacheza baada ya kupewa Kadi Nyekundu walipocheza na Deportivo La Coruna.
Barcelona watamkosa Kiungo Xavi ambae ni majeruhi na pia Nyota wao Lionel Messi anatarajiwa licha ya majuzi kukosa mazoezi aliporitiwa anaugua homa.
TATHMNI YA MECHI:
Mechi ya kwanza ya La Liga Msimu huu kati ya Mahasimu hawa iliyochezwa hapo Oktoba 7 huko Nou Camp ilimalizika kwa Bao 2-2 huku Nyota Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakifunga Bao 2 kila mmoja kwa Timu zao.
Akiongelea Mechi hii, Kocha Msaidizi wa Barcelona Jordi Roura, ambae ndie ameshika hatamu kwa kukosekana Kocha wao Tito Vilanova ambae ni mgonjwa, amesema: “Tulipocheza na AC Milan na Real hatukuwa na cheche zetu na hili lisituvunje moyo. Leo, Timu itajituma na kushindana kwa kila kitu.”
Roura alikiri kuwa Wachezaji wake wameumizwa na vipigo vya 2-0 toka kwa AC Milan na 3-1 toka kwa Real na pia alimtetea Nyota wao Lionel Messi alieshindwa kufurukuta kwenye Mechi hizo mbili ambazo alishindwa hata kupiga Shuti moja lililolenga Golini na hiyo ni mara yake ya kwanza kwa kitu hicho kumtokea Msimu huu.
Kambi ya Real haijazungumza lolote kuhusu Mechi ya leo lakini inaaminika Kocha Jose Mourinho huenda akapangua Kikosi chake cha leo kwa vile wameshakata tamaa kutetea Taji lao la La Liga na pia Jumanne wana Mechi ngumu ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Old Trafford dhidi ya Manchester United wanayotakiwa kuifuta sare ya 1-1 waliyotoka na Man United katika Mechi ya kwanza.
USO kwa USO:
COPA del REY 26 Feb: Barcelona 1 Real Madrid 3
COPA del REY Jan 30: Real Madrid 1 Barcelona 1
LA LIGA Okt 7: Barcelona 2 Real Madrid 2
SUPERCOPA Ago 29: Real Madrid 2 Barcelona 1
SUPER COPA Ago 23: Barcelona 3 Real Madrid 2
DONDOO za KUMBUKUMBU:
Real Madrid
-Wameshinda Mechi zao 10 kati ya 11 zilizopita walizocheza Nyumbani na hawajafungwa katika Mechi 24 zilizopita.
-Msimu huu Real wamefunga jumla ya Mabao 101 katika Mechi zao 42 hadi sasa.
Barcelona
-Wameshinda Mechi 3 tu kati ya 7 walizocheza mwisho katika Mashindano yote na kufungwa 2 na sare 2.
-Katika Mechi 7 walizocheza mwisho na Real Madrid, Barca wameshinda Mechi 1 tu na kufungwa 3 na sare 3.
VIKOSI VINAVYOTARAJIWA KUANZA:
REAL MADRID [Mfumo: 4-2-3-1]:
Diego López
Arbeloa • Sergio Ramos • Pepe • Marcelo
M. Essien • L. Modrić
José Callejón • Kaká • Cristiano Ronaldo
K. Benzema
BARCELONA [Mfumo: 4-3-3]:
Valdés
Dani Alves • Piqué • J. Mascherano • Jordi Alba
Xavi • Busquets • Iniesta
Pedro • L. Messi • David Villa
Refa: Miguel Pérez‎
LA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Machi 1
Getafe 2 Real Zaragoza 0
Jumamosi Machi 2
Real Madrid CF v FC Barcelona [SAA 12 JIONI]
Deportivo La Coruna v Rayo Vallecano
Osasuna v Athletic de Bilbao
Valencia v Levante
Jumapili Machi 3
Granada CF v Real Mallorca
RCD Espanyol v Real Valladolid
Malaga CF v Atletico de Madrid
Real Sociedad v Real Betis
Jumatatu Machi 4
Sevilla FC v Celta de Vigo

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video