Jumamosi, 09 Machi 2013 09:35
STRAIKA
wa Bayern Munich Mario Mandzukic amesema wao nia yao ni ‘kupasha moto’
kwa kuifunga Fortuna Duesseldorf leo kwenye Bundesliga yakiwa ni
matayarisho yao kwa ujio wa Arsenal hapo Jumatano Uwanjani Allianz Arena
ikiwa ni Mechi ya Marudiano ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI huku Bayern
wakiwa kifua mbele baada ya kuifumua Arsenal Bao 3-1 katika Mechi ya
kwanza iliyochezwa Emirates Wiki mbili zilizopita.
+++++++++++++++++++++++++++
BUNDESLIGA
Ijumaa Machi 8
FC Augsburg 1 FC Nuremberg 2
Jumamosi Machi 9
Bayern Munich v Fortuna Dusseldorf
Schalke 04 v BV Borussia Dortmund
SC Freiburg v VfL Wolfsburg
FSV Mainz 05 v Bayer 04 Leverkusen
SpVgg Greuther Furth v TSG Hoffenheim
Borussia Mönchengladbach SV v Werder Bremen
Jumapili Machi 10
Hannover 96 v Eintracht Frankfurt
VfB Stuttgart v Hamburger SV
+++++++++++++++++++++++++++
Kwenye Bundesliga, huku Mechi zikiwa
zimebaki 10, Bayern Munich wako kileleni wakiwa Pointi 17 mbele ya Timu
ya Pili, Mabingwa watetezi Borussia Dortmund.
+++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 24]
Bayern Munich Pointi 63
BV Borussia Dortmund 46
Bayer 04 Leverkusen 45
Eintracht Frankfurt 38
SC Freiburg 36
Schalke 04 36
Hamburger SV 35
FSV Mainz 05 34
Borussia Mönchengladbach 34
+++++++++++++++++++++++++++
Mara ya mwisho kwa Fortuna Dusseldorf
kuifunga Bayern ilikuwa ni Aprili 1991 na Mechi zote 3 zilizofuata
Bayern walishinda bila kufungwa hata Goli moja.
Hata hivyo, Mandzukic amesema wanaiheshimu Fortuna lakini wao wako tayari kuikabili.
Aliongeza: “Tuko nyumbani na tunataka
kuongeza wimbi letu la ushindi. Wengi wanafikiri tushaingia Robo Fainali
ya UCL lakini lolote linaweza kutokea kwenye Soka.”
Mandzukic alifunga Bao la 3 wakati
Bayern ilipoipiga Arsenal 3-1 na Bao nyingine zao kufungwa na Kroos na
Muller wakati la Arsenal lilifungwa na Podolski.
Wakiwa tayari wametinga Robo Fainali ya
UCL baada ya kuifunga Shakhtar Donetsk, Mabingwa Borussia Dortmund
wanasafiri Kilomita 40 kucheza na Jirani zao Schalke 04 ambao wameshinda
Mechi moja tu kati ya 5 za Bundesliga walizocheza na Dortmund na hiyo
ya ushindi ni Bao 2-1 walioupata nyumbani kwa Dortmund Uwanja wa Signal
Iduna Park Mwezi Oktoba Mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment