Friday, March 8, 2013

KIPA namba moja wa Yanga, Ally Mustafa Mtinge ‘Barthez’ aliyekuwa mgonjwa, amepona na leo amefanya mazoezi na wenzake tayari kusimama langoni kesho timu yake ikimenyana na Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Barthez aliye katika msimu wake wa kwanza Yanga SC tangu asajiliwe kutoka kwa mahasimu, Simba SC, jana alishindwa kufanya mazoezi kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya tumbo, lakini amedamka Kijitonyama na kujifua.
Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema kwamba, Barthez ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwepo mzoezini asubuhi  wakifanya maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo wa kesho.
Aidha, Kizuguto alisema kiungo Nurdin Bakari pia naye amefanya mazoezi leo na kwamba mchezaji pekee ambaye hakufanya mazoezi ni beki Juma Abdul anayesumbuliwa na homa.
Kizuguto alisema baada ya kufanyiwa vipimo juzi, imegundulika Nurdin hana maumivu makubwa na hatafanyiwa tena upasuaji wa goti. Alisema mpango wa beki Ladislaus Mbogo kufanyiwa upasuaji wa uvimbe kwenye shavu lake upo pale pale, na zoezi hilo litafanyika kati ya Jumatatu na Jumatano wiki ijayo.
Yanga iliiingia kambini jana, katika hosteli za klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Toto.
Yanga inaongoza Ligi Kuu kwa sasa kwa pointi zake 42, baada ya kucheza mechi 18, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 36, baada ya kucheza mechi 18 pia, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 31 sawa na Coastal Union ya Tanga na Mtibwa Sugar ya Morogoro wanashika nafasi ya tatu, wakibebwa na wastani wao mzuri wa mabao.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video