Saturday, March 9, 2013

BARCA_VICHWA_CHININDIO KWANZA wakiwa wanatoka kwenye visago mfululizo, Vinara wa La Liga Barcelona, leo Jumamosi wapo nyumbani kucheza na Timu inayosuasua Deportivo La Coruna kwenye Ligi huku Jumanne wakikabiliwa na Mechi ngumu ya marudiano na AC Milan kwenye UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI wakisaka kupindua kipigo cha Bao 2-0 ili kutinga kuingia Robo Fainali.
Vipigo mfululizo kwa Barca ni hicho cha AC Milan na viwili toka kwa Mahasimu wao Real Madrid, likiwa ni wimbi bovu kwao tangu walipoanza kuwika Mwaka 2008 chini ya Kocha wao wa zamani Pep Guardiola.
Akiongelea hali hiyo, Supastaa wao, Lionel Messi, ametamka: “Tunatoka kwenye vipigo vikubwa na sasa lazima tutumie nguvu zaidi kuibadilisha hali hii. Tunajua Mechi na Milan ndio ufunguo wetu!”
Hadi sasa Barcelona wapo kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 11 mbele ya Timu ya Pili Atletico Madrid na safari hii mpinzani wake, Deportivo La Coruna, wako mkiani wakiwa hawajashinda hata Mechi moja ugenini.
Jumapili, Atletico Madrid watakuwa kwao Uwanja wa Vicente Calderon ambako wamecheza Mechi 13 za Ligi na kushinda zote lakini safari hii wageni wao ni Timu ngumu Real Sociedad ambayo hivi sasa imekuja juu.
Real Madrid, ambao wanatoka kwenye wimbi kubwa la ushindi la kuifunga Barcelona mara mbili mfululizo na kuwabwaga nje ya UCL Manchester United na wao kutinga Robo Fainali, wanasafiri kwenda kucheza na Celta Vigo ambayo ni moja ya Timu za mkiani zilizo hatarini kuporomoka Daraja.
Real Madrid wako nafasi ya 3 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Atletico Madrid na Pointi 13 nyuma ya Vinara Barcelona.
RATIBA/MATOKEO:
LA LIGA
RATIBA
Ijumaa Machi 8
Real Betis v Osasuna
Jumamosi Machi 9
Rayo Vallecano v RCD Espanyol
Real Valladolid  v Malaga CF
FC Barcelona v Deportivo La Coruna
Real Mallorca v Sevilla FC
Jumapili Machi 10
Athletic de Bilbao v Valencia
Levante v Getafe CF
Celta de Vigo v Real Madrid CF
Atletico de Madrid v Real Sociedad
SERIE A
Ijumaa Machi 8
Genoa 0 AC Milan 2
Jumamosi Machi 9
Udinese v AS Roma
Jumapili Machi 10
Atalanta v Pescara
Chievo Verona v Napoli
Juventus v Catania
Parma v Torino FC
Palermo v Siena
Cagliari v Sampdoria
Inter Milan v Bologna
SS Lazio v Fiorentina
BUNDESLIGA
Ijumaa Machi 8
FC Augsburg 1 FC Nuremberg 2
Jumamosi Machi 9
Bayern Munich v Fortuna Dusseldorf
Schalke 04 v BV Borussia Dortmund
SC Freiburg v VfL Wolfsburg
FSV Mainz 05          v Bayer 04 Leverkusen
SpVgg Greuther Furth v TSG Hoffenheim
Borussia Mönchengladbach SV v Werder Bremen
Jumapili Machi 10
Hannover 96 v Eintracht Frankfurt
VfB Stuttgart v Hamburger SV

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video