Monday, March 4, 2013

>>NI KLABU BORA DUNIANI, SASA MECHI 3, VIPIGO 3 VITAKATIFU!!
BARCA_VICHWA_CHINI>>WAMETWANGWA 2-0 NA AC MILAN, REAL WAIPIGA 3-1 & 2-1!
>>’TIKI TAKA’ IMEKUWA ’TAKA TAKA’????
NDANI YA MIAKA MINNE, chini ya Kocha Pep Guardiola, FC Barcelona walitwaa Makombe 14 kati ya 19 waliyoshindania, leo hii Dunia imeshuhudia kwa kipindi kifupi tu ikipoteza Mechi kubwa 3 mfululizo kwa kuchapwa 2-0 na AC Milan kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na kuwekwa hatihati kufuzu kwao, kupigwa 3-1 na Real Madrid, tena wakiwa kwao Nou Camp na kutupwa nje ya COPA del REY Kombe ambalo ndio walikuwa Mabingwa, na kupigwa tena na Real Bao 2-1 Siku kadhaa baadae kwenye La Liga.
Matokeo hayo, kwa Klabu inayosifiwa ndio Bora Duniani, ikiwa na Mchezaji Bora Duniani, Lionel Messi, Viungo Bora Duniani, Xavi Hernández na Andres Iniesta, ni kitu cha kustua sana kwa Wadau wao.
NINI KIMEJIRI NOU CAMP??
Baadhi ya Wachambuzi wanahisi ni mabadiliko ya Kocha pale alipoondoka Pep Guardiola naMESSI-MASHAKANI mikoba kuchukuliwa na Tito Vilanova, ambae hata hivyo, hivi karibuni hakuwepo Benchi kwa vile ni Mgonjwa, lakini wapo wanaoamini kushuka kwa viwango vya Uchezaji wa Viungo Xavi Hernández na Andres Iniesta, ambao ndio uti wa mafanikio ya Barca, kumezaa Timu kucheza bila ile presha iliyozoeleka ya Staili ya “Tiki Taka.”
Lakini pia wapo waliotoa nadharia kwamba Timu nyingi Siku hizi zishabaini Staili ya Barca na hilo limewafanya Barca wenyewe wabadili Staili yao na matokeo yake kuonekana ni Timu ya kawaida tu na kutoa mwanya kwa wao kufungwa.
Hao, wanadai, mara baada ya Msimu uliopita Mwezi Aprili kufungwa na Chelsea na Real kwa Staili ya ‘Kupaki Basi’, Barca waliamua kutafuta njia mbadala ya kuziponda Timu za Staili hiyo ya ‘Basi’ kwa kupanua Uwanja tofauti na huko nyuma walipokuwa wakijikusanya kwa pamoja, kucheza pasi fupi fupi, haraka haraka na kuzichosha Timu kwa “Tiki Taka”, na hili limewafanya wao wenyewe wawe dhaifu kwa Wapinzani kufanya Kaunta Ataki ya haraka wanapopoteza Mpira.
Matokeo yake, Msimu huu, Barca wamekuwa wakifungwa Bao nyingi kupita Siku za nyuma.
Pia hii Staili yao mpya imewabadilisha kina Xavi na Iniesta ambao huko nyuma walikuwa wakishuka nyuma kupokea mipira na kumlisha Messi aliekuwa mara zote yuko karibu na eneo la hatari, Penati Boksi, ambako huleta madhara makubwa lakini sasa Messi mwenyewe anawajibika kurudi nyuma kusaka mipira huku Timu ikilazimika kila mpira kumpa yeye ili ajenge mashambulizi na hilo limepoteza madhara yake Golini.
Lakini Barca wana nafasi kubwa ya kuwanyamazisha wale wanaodai zama zao ziko ukingoni ikiwa tu watapindua kipigo cha 2-0 mikononi mwa AC Milan na wao kutinga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Timu hizi zitakaporudiana hapo Jumanne Machi 12 Uwanjani Nou Camp.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video