Thursday, March 14, 2013

Kutoka kwa Bin Zubeiry

Baadhi ya wachezaji wa Azam FC

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC jana wamefika salama mjini Monrovia, Liberia tayari kwa mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya michuano hiyo, dhidi ya wenyeji Barrack Young Controllers.
Azam FC iliyoondoka jana na kufika jana hiyo hiyo, imetua nchini humo na kikosi cha wachezaji 22, ambao ni makipa; Mwadini Ally na Aishi Manula, mabeki; Joackins Atudo (Kenya), David Mwantika, Himid Mao, Malika Ndeule, Waziri Salum na Luckson Kakolaki.
Kwa upende wa viungo ni Abdulhalim Humud, Kipre Balou (Ivory Coast), Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Salum Abubakar, Humphrey Mieno (Kenya), Abdi Kassim ‘Babbi’, Uhuru Suleiman na Khamis Mcha ‘Vialli’ wakati washambuliaji ni John Bocco ‘Adebayor’, Kipre Tchetche (Ivory Coast), Seif Abdallah, Brian Umony (Uganda) na Gaudence Mwaikimba. 
Barrack Young Controllers iliyoanzishwa mwaka 1997, inatumia Uwanja wa Antonette Tubman uliopo mjini Monrovia kwa mechi zake na haina tofauti sana na Azam kihistoria. 
Wakati Azam ilianzishwa mwaka 2004 na kucheza Ligi Kuu ya nchi kwa mara ya kwanza mwaka 2008, hadi sasa ina mataji mawili ya Kombe la Mapinduzi na moja la Kombe la Hisani ya nchini DRC, wapinzani wao wana mataji mawili ya Kombe la Liberia na moja la Super Cup ya nchini humo.
Azam ni timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye michuano ya Afrika baada ya Simba na Jamhuri ya Pemba kutolewa katika Raundi ya Kwanza tu ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Azam inayofundishwa na Muingereza Stewart John Hall, ilifuzu kuingia Raundi ya Pili baada ya kuichapa jumla ya mabao 8-1 Al Nasir Juba ya Sudan. 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video