Tuesday, March 5, 2013

Na Baraka Adson, Dar es salaam

Klabu ya African Lyon ya jijini Dar es salaam inataraji kushuka dimbani kesho kukabiliana na vijana machachari wa Charles Boniface Mkwasa "Master", maafande wa Ruvu shooting ya MKoani Pwani katika uwanja wa kisasa wa klabu ya Azam fc Lambalamba, Chamazi Complex majira ya saa kumi kamili alasari.
Kuelekea katika mchezo huo mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo mkenya Charles Otieno ameiambia MATUKIO DUNIANI  kuwa mchezo huo ni mgumu sana kwao kutokana kusumbuliwa mara nyingi na Ruvu shooting.

"Ruvu shooting ni wababe wetu mara kwa mara japokuwa huwa wanatufunga 1-0 na sio mbili, kwa mchezo wa kesho ni muhimu kwetu kwani tunahitaji pointi tatu katika harakati zetu za kuepuka kushuka daraja, na Shooting wanasaka alama tatu muhimu kupata nafasi nzuri katika msimamo, lakini tutapambana kushinda mchezo huo". Otieno alisema.

Pia mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kwa msimu huu African Lyon tatizo lake kubwa ni kushindwa kutengeneza nafasi za kufunga na hata kama watafanikiwa kutengeneza nafasi huwa wanashindwa kutumia.

"Tuna tatizo la kushindwa kutengeneza nafasi za kufunga na hata kama tukitengeneza washambuliaji wetu hawako makini kuzitumia, nadhani kilichobaki ni kupigania kubaki ligi kuu ili tujipange upya msimu ujao". alisisitiza Otieno.

Kwa upande wa wapinzani wao, Ruvu shooting, kupitia kwa afisa habari wake mwenye maneno mengi Masau Bwire wametamba kuwachabanga Africa Lyon kwa mara yingine tena.

Masau alisema kikosi chao kipo safi na kimefanya mazoezi makubwa hivyo watautumia mchezo huo wa kesho kama mazoezi ya kukabiliana na Yanga mwishoni mwa wiki hii.

"African Lyon ni wateja wetu, hatutumia nguvu kujiandaa dhidi yao kwani lazima wafungwe tu, sisi hesabu zetu ni kuwakabili wazee wa uturuki, klabu ya Yanga baada ya mechi ya kesho"

"Ruvu shooting kuifananisha na Lyon ni sawa na kulinganisha Tembo na Sungura, hawana makeke ya kutufunga sisi". Masau alijigamba.

Hata hivyo msemaji huyo aliongeza kuwa kikosi chao kitaingia Dar es salaam leo hii tayari kwa kuzoeza hali ya hewa ya jijini hili.

Michezo Mingine kesho itakuwa baina ya JKT Oljoro dhidi ya Tanzania Prisons katika dimba la Sh. Amri Abeid jijini Arusha, kuku Mgambo JKT wakiwa nyumbani kwao Mkwakwani wataumana na wakata miwa wa Mtibwa sugar katika dimba lao la Ccm Mkwakwani jijini Tanga.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video