>>KAMA KAWA, BALOTELLI APIGA BAO!
AC Milan jana Usiku ilishinda Bao 2-0
ilipocheza Mechi ya Serie A ugenini na Genoa na kujizatiti nafasi ya 3
wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Napoli hii ikiwa ‘pashamoto’ ya mtanange wao
wa Marudiano ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, huko Nou Camp hapo Jumanne
huku wao wakiwa Washindi wa Bao 2-0 katika Mechi ya kwanza.
+++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 27 isipokuwa inapotajwa]
Juventus Pointi 59
Napoli 53
AC Milan Mechi 28 Pointi 51
Inter Milan 47
SS Lazio 47
Fiorentina 45
AS Roma 43
Catania 42
+++++++++++++++++++++
Bao za AC Milan zilifungwa katika kila
Kipindi na la kwanza kupitia Giampaolo Pazzini na la pili la Mario
Balotelli alieingizwa toka Benchi.
Katika Mechi hii, AC Milan walimaliza
Mtu 10 baada ya Beki wao Kevin Constant kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu
kufuatia Kadi za Njano mbili.
Ligi hiyo inaendelea leo kwa Mechi moja
tu kati ya Udinese na AS Roma na Jumapili zipo Mechi kibao zikiwemo za
Mabingwa na Vinara Juventus kuivaa Catania na Napoli kucheza ugenini na
Chievo Verona.
SERIE A
Ijumaa Machi 8
Genoa 0 AC Milan 2
Jumamosi Machi 9
Udinese v AS Roma
Jumapili Machi 10
Atalanta v Pescara
Chievo Verona v Napoli
Juventus v Catania
Parma v Torino FC
Palermo v Siena
Cagliari v Sampdoria
Inter Milan v Bologna
SS Lazio v Fiorentina
0 comments:
Post a Comment