BARAZA
la Sanaa la Taifa (BASATA) limewapongeza waandaaji wa tamasha la kila
mwaka la Pasaka, Msama Promotions kwa kulifanya tukio hilo kuwa la
kimataifa kwa kushirikisha waimbaji kutoka nchi mbalimbali.
Akizungumza hivi karibuni katika
tathimini ya tamasha la mwaka jana lililofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Basata Ilala jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mfuko wa
Uwezeshaji, Angelu Luhala alisema inapendeza kuona jambo hilo linakuwa
la Afrika badala ya Afrika Mashariki kama ilivyo hivi sasa.
Luhala alitaka waandaaji hao
kuongeza umakini na kuongeza waimbaji kutoka mikoa mingi zaidi tofauti
na sasa kwa vile linavuta hisia za watu wengi katika muziki wa Injili
wenye maushui ya kumtukuza Mungu.
Naye Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa,
Nsao Shalua licha ya kuipongeza kampuni hiyo ya Msama Promotions kwa
ubunifu wa tukio hilo, pia aliisifu kwa kuzingatia sheria na taratibu za
baraza hilo ambalo ndio dira ya sanaa Tanzania.
Aliwataka kuwasilisha mapema
tathimini ya maandalizi ya mwaka jana ili kufanikisha tamasha lijalo.
Naye shabiki wa tamasha hilo, Eunice Muhandia alisema waandaaji wa
tamasha hilo wanatakiwa kuweka umakini katika suala la tiketi kwa
sababu mwaka jana ilikuwa shida ndani ya uwanja wa taifa.
KUTOKA FULLSHANGWE
0 comments:
Post a Comment